Ni udanganyifu gani ulishawahi kuufanya katika chumba cha mtihani ulipokuwa mwanafunzi?

secretarybird

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2024
Posts
2,998
Reaction score
4,948
Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu(99.9) humu JF tumepita shuleni kwani tusingepita kule tusingekuwa na uwezo wa kutoa wala kusoma comments humu. Mfumo wetu wa elimu unamtaka mwanafunzi wafaulu mtihani kwani mtihani ndio unaomfanya mtu kutoka ngazi moja kwenda nyingine endapo atafaulu ama aachane na shule (kufeli).

Sasa katika harakati za kuupambania ufualu wanafunzi wanajaribu kufanya hila yoyote ilimradi wafaulu ili waendelee mbele au kukwepa bakora za mwalimu wa somo.

Binafsi nilikuwa nina uwezo wa kuangalia majibu ya mtu wa pembeni yangu bila kugeuza shingo yaani niliweza kuyageuza macho yangu ila shingo likabaki vile vile, kwa kifupimacho yangu yalikuwa kama yale matairi ya gari ya mbele.

Namshukuru mungu sikushtukiwa mpaka namaliza. Wewe ulifanya udanganyifu gani kipindi cha uanafunzi wako.

Sema na mungu wako atakusamehe.
 
   Sisi darasani tulikuwa na ushirikiano kwenye mtihani hasa ya kuchagua majibu ya a,b,c,d. Kama hujui swali unanyoosha kidole na kumwambia msimamizi Nisomee swali la 5,msimamizi atasoma kwa sauti akimaliza baada ya mda mwingine anayoosha kidole tena na kumwambia nisomee swali la tano D,atarudia kusoma hiyo D msimamizi bila kujua kumbe ndo anasoma jibu,basi wote mnajua jibu ndo hilo "D".

Halafu lingine Vifungo ya shati vinatumika kama a,b,c,d kama hujui jibu la swali la kuchagua msimamizi akiangalia tu pembeni unaonyesha namba ya swali kwa vidole,yule unayemwangalia anashika kifungo cha shati ambalo ni jibu, maana kifungo cha kwanza ni A, cha pili B, cha tatu C, cha nne D,yeye anaishika tu kama anaifunga.
 
Mimi nliwahi mpa mtu majibu hatimae kenge Ile ikanipita tena ilinipita mbali sana wakati mie sasa nilipotea mbali sanaaa
Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigusi pepa) nilipohakikisha maswali yote kayajaza nikajifanya nakagua kazi yangu kumbe ndo naweka majibu yaliyosahihi tofauti aliyoyaandika yeye.
Kwenye ule mtihani jamaa alipata sifuri na alinichukia mno kwa kumpoteza maboya.

NILIMKOMESHA.
 
   Sisi darasani tulikuwa na ushirikiano kwenye mtihani hasa ya kuchagua majibu ya a,b,c,d. Kama hujui swali unanyoosha kidole na kumwambia msimamizi Nisomee swali la 5,msimamizi atasoma kwa sauti akimaliza baada ya mda mwingine anayoosha kidole tena na kumwambia nisomee swali la tano D,atarudia kusoma,basi wote mnajua jibu ndo hilo "D".

Halafu lingine Vifungo ya shati vinatumika kama a,b,c,d kama hujui jibu la swali la kuchagua msimamizi akiangalia tu pembeni unaonyesha namba ya swali kwa vidole,yule unayemwangalia anashika kifungo cha shati ambalo ni jibu, maana kifungo cha kwanza ni A, cha pili B, cha tatu C, cha nne D,yeye anaishika tu kama anaifunga.
Duh! mwanafunzi kwa utundu......
 
Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigusi pepa) nilipohakikisha maswali yote kayajaza nikajifanya nakagua kazi yangu kumbe ndo naweka majibu yaliyosahihi tofauti aliyoyaandika yeye.
Kwenye ule mtihani jamaa alipata sifuri na alinichukia mno kwa kumpoteza maboya.

NILIMKOMESHA.
Sisi tulikuwa tunatumia viungo vya mwili mfano sijui ni C, pia ni B, D jicho.
 
Huo sio uchoyo mkuu.
 
Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigus
NILIMKOMESHA.
Kwenye mtihani kuna heka heka nyingi sana,niliingia na daftari kabisa,msimamizi akanishtukia daftari lilikuwa ndani ya dawati,ile anakuja akosea akaangalia pembeni nikaitoa kwenye dawati nikakalia,alipofika alifungua dawati akakuta hamna kitu akaondoka,mara ya pili macho yakakutana tena,nikasema huyu sasa atasema nisimame ashaangalia dawati,nikaitoa nikairudisha ndani ya dawati,alipofika akaniambia simama akakuta hamna kitu,akaniambia wewe kuna kitu ila nimeshindwa,sikufanya hiyo paper kwa amani
 
Niliwahi kufanya ujinga baada ya kumaliza mtihani nikalala kwenye dawati Hadi nikachoka nikaamua nichore chore kwenye mtihani wa maswali nikajikuta bonge la bus kubwa msimamizi akanifuma alinitisha sana et watanifutia matokeo siku hiyo nililia sana. Msimamizi alikuwa madam nilimubembeleza Hadi nikalala chini mwishoe kakanisamehe la saba hiyo 20....
 
Mi alinikuta naongea na mtu, hakusikia neno lakini aliona jinsia ndomo wangu ulivyokuwa Unacheze cheza, nilipoona msimamizi kaniona sikuacha kuchezesha midomo mithili ya mbuzi anayebugia majani mpaka aliponifikia, nilifanya hivyo ili adhani kuwa nilikuwa nafanya tu kuchezesha midomo. Nilichezesha midomo hiyo siku hadi nika maliza mtihani mpaka misuli midomo ikachaka😂😂😂
 
I guess ulikuwa kwenye mtihani wa hesabu.
 
Mi alinikuta naongea na mtu, hakusikia neno lakini aliona jinsia ndomo wangu ulivyokuwa Unacheze cheza, nilipoona msimamizi kaniona sikuacha kuchezesha midomo mithili ya mbuzi anayebugia majani mpaka aliponifikia, nilifanya hivyo ili adhani kuwa nilikuwa nafanya tu kuchezesha midomo. Nilichezesha midomo hiyo siku hadi nika maliza mtihani mpaka misuli midomo ikachaka😂😂😂
Aisee kwenye mtihani wa Mock au Taifa wale wasimamizi ukijichanganya tu hawana huruma maana wakuwaga wametoka mbali sio wa sehemu husika.
 
Nakumbuka kipindi nipo form one nilikuwa na rafiki yangu saidi tuliamua kuingia na daftari kabsa kwenye Mtihani wa chemistry, na tulifanikiwa kuingia nalo tukaliweka chini ya dawati letu bahati nzuri tulikuwa tunakaa bakabecha sasa cha kushanganza tulikuwa tunafunua daftari kwa vidole vya miguu au unajifanya umeangusha kalamu ili kupata nafasi la kulifunua daftari. Daah nikikumbuka Ile moment nachekaga tu.
 
Back
Top Bottom