Ni udanganyifu gani ulishawahi kuufanya katika chumba cha mtihani ulipokuwa mwanafunzi?

Nakumbuka kipindi nipo form one nilikuwa na rafiki yangu saidi tuliamua kuingia na daftari kabsa kwenye Mtihani wa chemistry, na tulifanikiwa kuingia nalo tukaliweka chini ya dawati letu bahati nzuri tulikuwa tunakaa bakabecha sasa cha kushanganza tulikuwa tunafunua daftari kwa vidole vya miguu au unajifanya umeangusha kalamu ili kupata nafasi la kulifunua daftari. Daah nikikumbuka Ile moment nachekaga tu.
Yawezekana wewe umepewa kipawa cha kupiga kinanda kwa kutumia vidole vya miguu sema hujajitambua tu. Kama uliweza kufungua safari kwa miguu sembuse kinanda.

Unapopewa kipaji jaribu kuitumia vema uihudumie jamii yako.
 
Ulikua ndo mtihani wa mwisho (ile mitihani ya kuandika majina) tukiumaliza tu huo mtihani tunafunga shule hadi January msimamizi alikua ametoka shule nyingine sasa masaa mawili ya mtihani yakaisha msimamizi akatuzuia kuendelea kuandika mi nikaendelea kutiririka kama dakika 5 nilivyooenda ku submit booklet jamaa akakataa kupokea booklet yangu ila zile booklet za wanafunzi wengine amezipanga mezani.

Nikaangalia huku na kule sikuona mwanafunzi mwenzangu yoyote karibu nikamuuliza unalifahamu jina langu? Akanijibu "silifahamu" alivyonijibu tu hivyo nikafunua zile booklet karibu 30 nikaweka booklet yangu katikati ya zile booklet zingine alaf nikapotea chap.
 
Wakati nipo chuo nilishawahi fanya mitihani miwili 🤣🤣🤣, ila Pesa acha tu. Kuna dingi moja lilikuwa linafanya kazi shirika X serikalini tulikuwa tunasoma naye. Sasa yule mzee darasani chenga. Sasa, akaniambia nimsaidie ananipa 100k, halafu ilikuwa test 2. Nikaona isiwe kesi nikamwambia asiandike chochote. Tulikaa karibu, nikaanza paper lake. Nikapiga nikamaliza, nikampasia. Nikaanza kufanya wa kwangu, nikapiga ile nakaribia kumaliza, timeout. Nikakusanya hivyohivyo kikubwa pesa.
 
Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigusi pepa) nilipohakikisha maswali yote kayajaza nikajifanya nakagua kazi yangu kumbe ndo naweka majibu yaliyosahihi tofauti aliyoyaandika yeye.
Kwenye ule mtihani jamaa alipata sifuri na alinichukia mno kwa kumpoteza maboya.

NILIMKOMESHA.
Alafu mnalalamika CCM Wana roho mbaya na mbinu chafu, kumbe watu mmefuzu toka zamani Kwa ujanja.😁😁👍
 
Wakati nipo chuo nilishawahi fanya mitihani miwili 🤣🤣🤣, ila Pesa acha tu. Kuna dingi moja lilikuwa linafanya kazi shirika X serikalini tulikuwa tunasoma naye. Sasa yule mzee darasani chenga. Sasa, akaniambia nimsaidie ananipa 100k, halafu ilikuwa test 2. Nikaona isiwe kesi nikamwambia asiandike chochote. Tulikaa karibu, nikaanza paper lake. Nikapiga nikamaliza, nikampasia. Nikaanza kufanya wa kwangu, nikapiga ile nakaribia kumaliza, timeout. Nikakusanya hivyohivyo kikubwa pesa.
Wewe Sasa hivi Kwa nafasi yako unaweza kuuza nchi au kuchukua 20% ili mladi umepata chako. Kumbe janja ya kupenda pesa ukianza zamani uko tayari upate marks kiduchu lakini upate mzigo.
 
Nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigusi pepa) nilipohakikisha maswali yote kayajaza nikajifanya nakagua kazi yangu kumbe ndo naweka majibu yaliyosahihi tofauti aliyoyaandika yeye.
Kwenye ule mtihani jamaa alipata sifuri na alinichukia mno kwa kumpoteza maboya.

NILIMKOMESHA.
Ahahahahh 🤣 🤣 🤣
 
Wewe Sasa hivi Kwa nafasi yako unaweza kuuza nchi au kuchukua 20% ili mladi umepata chako. Kumbe janja ya kupenda pesa ukianza zamani uko tayari upate marks kiduchu lakini upate mzigo.
Mkuu hawa wazee wanaotoka maofisini wanaenda kujiendeleza, hawa walikuwa watu wa faida sana kipindi kile nipo chuo. Sababu hawafanyi assignment, kwenye field/project report hawafanyi. Kwahiyo hapa ndo biashara ilipo. Ni kweli sometimes Performance yangu ilikuwa inadrop sababu ya pesa
 
Back
Top Bottom