Bwana Utam
JF-Expert Member
- Feb 15, 2016
- 19,559
- 36,514
Hehehe ila mwamba alikua vyema yaani anaibia kwa kuangalia pen tu Kuna watu wapo vyemaNilipokuwa shule ya msingi nilikuwa kichwa sana darasani kuna jamaa mmoja alikuwa hajui hata kusoma na alikuwa anangalia majibu kutoka kwangu. Siku mmoja aliangalia majibu kutoka kwangu lakini matokeo yaliporudi alinizidi kwa mbali akaanza kujigamba kwamba na yeye anajua na hapo ndipo nilipopata hasira nikaapa kutompa jibu na kwamba nitakuwa na ninakinga majibu kwa mkono kwani tulikuwa tunakaa kwenye dawati moja, mtihani uliofuata nilifanya hivyo (nilikinga majibu kwa mkono) kumbe jamaa alikuwa mjanja kwani alikuwa anangalia movement ya kalamu na maswali ya shule ya msingi yalikuwa multiple choices hivyo ikawa rahisi kunikadiria, alinipita tena akajigamba kwa mara nyingine aise nilikasirika sana. Siku iliyofuata nikasema namkomesha nilikuwa najifanya naandika herufi ya jibu sahihi kumbe kalamu haifiki kwenye pepa huku namwangalia jamaa kisirisiri nikagundua kuwa ananifuatisha (kwa mfano kama jibu la swali la 1 ni A mimi najifanya naandika C kumbe kalamu yangu haigusi pepa) nilipohakikisha maswali yote kayajaza nikajifanya nakagua kazi yangu kumbe ndo naweka majibu yaliyosahihi tofauti aliyoyaandika yeye.
Kwenye ule mtihani jamaa alipata sifuri na alinichukia mno kwa kumpoteza maboya.
NILIMKOMESHA.