Ni udanganyifu gani ulishawahi kuufanya katika chumba cha mtihani ulipokuwa mwanafunzi?

Yawezekana wewe umepewa kipawa cha kupiga kinanda kwa kutumia vidole vya miguu sema hujajitambua tu. Kama uliweza kufungua safari kwa miguu sembuse kinanda.

Unapopewa kipaji jaribu kuitumia vema uihudumie jamii yako.
 
Yawezekana wewe umepewa kipawa cha kupiga kinanda kwa kutumia vidole vya miguu sema hujajitambua tu. Kama uliweza kufungua safari kwa miguu sembuse kinanda.

Unapopewa kipaji jaribu kuitumia vema uihudumie jamii yako.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ bahati mbaya hicho kipaji sikukitambua mpaka muda huu.
 
Jamaa alinipasia pepa bahati mbaya Muhindi akanidaka. Akantoa nje.

Halafu akarudi kwa jamaa yangu akamuuliza,

Mhindi : "Why did you give him your paper?"

Jamaa : "Because he is stupid."

Mhindi : "You are stupid too man, Get out Get Out"


Yule jamaa miyeyusho sana.
 
Ulikua ndo mtihani wa mwisho (ile mitihani ya kuandika majina) tukiumaliza tu huo mtihani tunafunga shule hadi January msimamizi alikua ametoka shule nyingine sasa masaa mawili ya mtihani yakaisha msimamizi akatuzuia kuendelea kuandika mi nikaendelea kutiririka kama dakika 5 nilivyooenda ku submit booklet jamaa akakataa kupokea booklet yangu ila zile booklet za wanafunzi wengine amezipanga mezani.

Nikaangalia huku na kule sikuona mwanafunzi mwenzangu yoyote karibu nikamuuliza unalifahamu jina langu? Akanijibu "silifahamu" alivyonijibu tu hivyo nikafunua zile booklet karibu 30 nikaweka booklet yangu katikati ya zile booklet zingine alaf nikapotea chap.
 
Wakati nipo chuo nilishawahi fanya mitihani miwili 🀣🀣🀣, ila Pesa acha tu. Kuna dingi moja lilikuwa linafanya kazi shirika X serikalini tulikuwa tunasoma naye. Sasa yule mzee darasani chenga. Sasa, akaniambia nimsaidie ananipa 100k, halafu ilikuwa test 2. Nikaona isiwe kesi nikamwambia asiandike chochote. Tulikaa karibu, nikaanza paper lake. Nikapiga nikamaliza, nikampasia. Nikaanza kufanya wa kwangu, nikapiga ile nakaribia kumaliza, timeout. Nikakusanya hivyohivyo kikubwa pesa.
 
Alafu mnalalamika CCM Wana roho mbaya na mbinu chafu, kumbe watu mmefuzu toka zamani Kwa ujanja.πŸ˜πŸ˜πŸ‘
 
Wewe Sasa hivi Kwa nafasi yako unaweza kuuza nchi au kuchukua 20% ili mladi umepata chako. Kumbe janja ya kupenda pesa ukianza zamani uko tayari upate marks kiduchu lakini upate mzigo.
 
Ahahahahh 🀣 🀣 🀣
 
Wewe Sasa hivi Kwa nafasi yako unaweza kuuza nchi au kuchukua 20% ili mladi umepata chako. Kumbe janja ya kupenda pesa ukianza zamani uko tayari upate marks kiduchu lakini upate mzigo.
Mkuu hawa wazee wanaotoka maofisini wanaenda kujiendeleza, hawa walikuwa watu wa faida sana kipindi kile nipo chuo. Sababu hawafanyi assignment, kwenye field/project report hawafanyi. Kwahiyo hapa ndo biashara ilipo. Ni kweli sometimes Performance yangu ilikuwa inadrop sababu ya pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…