Ni ujenzi gani wa kisasa ambao wewe binafsi haupendelei?

Ni ujenzi gani wa kisasa ambao wewe binafsi haupendelei?

Joined
Dec 13, 2022
Posts
11
Reaction score
43
First of all, heshima kwa wote waliojenga.

Hoja zangu hazimaanishi kuwakosoa ila ni kutofautiana na mapendeleo.

Mimi binafsi sipendelei aina ya ujenzi ufuatayo:

■ Uongezaji kimo wa nyumba kwa kuweka bati nyingi kuelekea juu sana.
Wanasema mfumo huu unasaidia kupunguza joto ndani ya nyumba. Ila kwa upande wangu sipendelei nyumba inapoongezeka urefu kwa mfumo wa paa. Lakini pia gharama inaongezeka kwa maana utatumia bati nyingi.

■ Nakshi na urembo mwingi kwenye gypsum board.
Napendelea kuona gypsum board ikiwa flat kawaida au kuwa designed kwa kiasi. Kusema kweli ukataji wa maumbo na uwekaji rangi tifauti na taa sio pendeleo langu.

■ Uwekaji wa paa juu ya geti kuu la nyumba.
Kwa upande wangu kama ni urembo nataka kudesign kwenye geti na niko under budget ninge prefer kuongezea nguvu katika uimara wa geti na kuweka security wires juu ya ya fensi.

■ Urembo na nakshi nyingi katika geti la nyumba.
Sivutiwi na uwekaji wa maua na maumbo mengi katika geti. Pia uwekaji wa rangi mchanganyiko katika geti sio fan kabisa. A simple designed large gate is fine to me.

■ Design ya kutengeneza uwazi katika uzio wa nyumba.
Naona kama hii design siku hizi imepungua. Mimi binafsi napendelea privacy. Nisingependa mtu anapopita anaona madhari ya ndani ya fensi kwa uwazi mkubwa. Napendelea fensi (sio ndefu sana), isiokuwa na uwazi.

Vipi kuhusu wewe, ni aina gani wa ujenzi wa kisasa usioupendelea?
 
Minyaa ndio kila kitu.
Mkuu, usinikumbushe gundi ya minyaa ilivyonitesa utotoni. Nilikuwa naitumia kutengenezea magari ya maboksi.
Ikishaingia machoni, unapelekwa kwa mama anayenyonyesha akukamulie maziwa kwenye macho ndio upone.

Umenikumbusha mbali mno.
Ukiachilia mbali kuingia machoni, Kuna Ile utomvu wake Bahati mbaya ukigusa ulimi au mdomoni, majanga matupu. tumeitumia sana kama gundi kutengeneza magari ya mabox.
 
Tatizo la Tanzania ni ustaarabu 0, ukiacha wazi bila geti utakutana na maajabu.

Ila itafika wakati watu watavunja na kuacha open space
Cheki wenzetu USA walivyo wastaarabu nyumba hazina ukuta wa fence wala mageti
images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom