Ni ujenzi gani wa kisasa ambao wewe binafsi haupendelei?

Ni ujenzi gani wa kisasa ambao wewe binafsi haupendelei?

Cheki wenzetu USA walivyo wastaarabu nyumba hazina ukuta wa fence wala mageti
View attachment 2476071
Tunaweka ma ukuta kuzuia vibaka wa kuiba tv na redio, sasa uko majuu kibaka gani wa kuiba tv?

Majuu ni majuu tu, niliona kwenye movie ya kikorea, mtu akienda zake kumwagilia moyo, basi akilewa haruhusiwi kuendesha gari. Basi gari anaacha linaletwa na temporary drivers ( tho kuna jina wanawaida) gari linaletwa nyumbani kwa usalama kabisa.

Sasa hapa bongo hata fundi anaelitengeneza anaweza lichongea likaibwa, kwenye parking napo siku hizi sio salama. Mtu akinunua gari kila saa anachungulia kuona kama lipo. Bongoooo dah.
 
Hamna.kitu nachukia kama uzio wa ukuta alafu ukute mrefuu kama gereza vile.

Jambo lingine sipendi madirisha madogo na nondo kwenye madirisha ni kama gereza tu, pakiwaka moto huponii.

Napenda ukuta mfupi sana kama wa mita moja juu then uwe una nakshi cha chuma sasa kuja juu.
 
Madirisha ya aluminium tabia yake ya kupitisha hewa nusu dirisha.

Joto hili la Dar ni mateso
Hili suala lipo waz.unapopiga aluminium jua wewe dirisha lako ndio kudumu utalifubgua nusu aluminium kama hauna budget ya A.C ni mateso. Sema yanasaidia kwenye kuzuia vumbi.ndan ila aluminium mwenzake A.c
 
Cheki wenzetu USA walivyo wastaarabu nyumba hazina ukuta wa fence wala mageti
View attachment 2476071
Ulishaona watu asubuh wanakaa vibarazan na madera huku wanasukana? Bas huko wana utamadun wao.huku kama huna fensi kwamza kila siku hata usahau ndala nje jamaa wale wa machupa ni sweepers wanapitaga mitaaan alfajir alfajir hiv hata jua bado.chochot atachokiona nje ana assume anaokota analamba hata ndala.fensi africa ndio kila kitu.
 
Ujenzi wa partion za vyumba vingi viiingi sehemu ya Tv (Tv case)
Hayo madesign ya sasa hiv tv wall sijui mataa taa yatapitwa na muda sasa hiv
Tv inatakiw kwanza ifungwe ukutan tu pale pasiw na mataa taa kwanza una distracted kuona tv na yale mataa taa.naona mafund walivochachamaa kuyajenga hayo matv wall
 
Finishing yoyote ya nyumba ambayo haipigwi plasta.

1. Nyumba nyingi za Dar uswahilini hazijapigwa plasta sijui ni stail au umaskini....hovyo kabisa.

2. Ujenzi wa nyumba wa mawe ambao haupigwa plasta ....hovyo kabisa.

3. Ujenzi wa matofali yasiyojengewa Yale ya kupachika bila mota na baadaye kuacha hivyo hivyo....hivyo kabisa.

4. Unakuta kitu Lina Hela, linaishi Dar kwenye joto lakini linajenga nyumba fuuupi.....hovyo..hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom