Ni ujinga kunywa bia kwa fujo na kupiga misele kwa gari msimu huu wa sikukuu. Halafu January unauza hiyo gari kwa bei ya kutupwa ili ulipe kodi/ada.

G4N

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2014
Posts
4,283
Reaction score
9,925
Maandalizi ya kuufanya mwezi January kuwa mwezi dume, yanafanyika msimu huu wa sikukuu. Watu wanaponda mali kana kwamba wanakufa kesho ama wameagana kabisa na shida za dunia.

January inapofika inawakuta watu hao wako hoi bin taabani kiuchumi. Wataanza kuhaha kuuza hata kile kidogo walichofanikiwa kukivuna.

Mwezi January ndiyo utakuta kiwanja cha 10M kinauzwa 3M, nyumba imepauliwa inauzwa 16M, gari ya 20M inauzwa 4M, bodaboda mpya inauzwa laki 7.

Ni ushauri tu. Wala huna haja ya kutokwa povu.
 
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom