mimi ni shabiki wa Magu tu sio sisiem naomba niweke hilo wazi, magoli ya mkono hupitia dizaini hii msimamizi uchaguzi wa sisiem mgombea chadema! hii haifai ndo chanzo cha wabunge ZZK auwawe, Sanamu la Diamond, Bangi iruhusiwe nk. Wabunge hawa na wa viti maalum hulifanya bunge kuwa dhaifu na kuishindwa kuisimamia na kuidabisha Executive na hivyo kuifanya serikali kuabudiwa badala ya wao kuabudu wapiga kura waliowapata ridhaa kuhifadhi na kutumia kodi zao!
Tume ya uchaguzi kupitisha wabunge feki ni sumu ya maendeleo ila kuwatimua wakurugenzi kusimamia uchaguzi ni hoja bora ya karne hii kutoka kwa Genius Shangazi Fatma yule binti mwanasheria mzenj ni Genius peke yake nchi nzima ya Zenj anaemfuatia kwa akili nyingi ni Jecha alietangaza mshindi wa uchaguzi akiwa chini ya uvungu peke yake bila kamati wala kufuata taratibu,
ukweli mimi nimesoma Mlimani ile yenyewe basi nilikuwa nikidharau mno wazenji nikiamini they cannot think like us ila baadae nilimkubali mno Shangazi Fatma katika hoja ya wasimamizi wa uchaguzi wawe neutral bila hivyo sisiem kidedea kwa karne mia mbili!
kwa miaka 20 chadema wanakula msoto , wanapotezwa, wanakula risasi na mabomu ya machozi, wako mahakamani kesi bandika bandua, wanakula vumbi kuandamana mabarabarani na kupigwa mabuti na virungu na kulipa mafaini kama yote na kulala selo na kunyea ndoo na kufungwa jela na kunyolewa vipara huko jela kumbe issue ni ndogo tu, kuperuse SHERIA YA UCHAGUZI, kucheza na vifungu tu vingine vitolewe vingine viongezwe, just paper work!!just office desk work!! Shangazi noma sana!
Angalizo:
Hivi nchi masikini ya bongo ni nani aliewaloga? hivi ni nani kati yetu yuko ni mzawa haswa nchi hii imejaa wakimbizi kutoka pande zote za dunia wakijifanya wabongo haswa na wengine wakiwa na nyazifa za juu? siku moja nilifika ofisi ya mfuko wa jamii boss mmoja top manyota pale Benjamin Mkapa building nikaongea nae jina la Kikenya pronounciation ya Kikenya nikasema tumekwisha!!
Hivi ni nani mtanzania yuko neutral nchini Tanzania kufaa kufanya kazi bila upendeleo tume ya uchaguzi?nchi hii ina ubaguzi mkubwa mno ulioko mioyoni mwa wabongo watu wanafki mno sababu midomoni hawasemi ubaguzi zao!!! nchi ya maajabu na vituko inafundisha ujamaa viongozi wengi wanaishi kibepari! (kuiba mali ya umma) , nchi hii hakuna neutral person, wewe kama sio sisiem uko upinzani, waislam versus wakristo, wabara versus wa pwani na visiwani, wanawake versus wanaume, matajiri versus maskini, wasomi versus wasiosoma!! haya na ukabila umo pia bima wanyakyusa, tra wachaga mlimani wahaya, polisi waislam kibao elimu ya juu wakristo, nchi mbovu sana hii na unafki za watu zitafanya iwe nchi maskini kwa karne nyingi, nchi hii kazi kupakapaka rangi na kufunikafunika ujinga tu , ukiwa msimamizi wa uchaguzi mhaya mgombea mhaya versus muha unampitisha mhaya!!
jibu la angalizo ninalo ila lipo mbali!