Ni ujuzi (skill) gani ukiwa nayo huwezi kulala njaa kwa mwaka ujao 2023?

Ni ujuzi (skill) gani ukiwa nayo huwezi kulala njaa kwa mwaka ujao 2023?

1- Ukipika chakula kizuri na ukazingatia usafi, hautolala njaa.

2- Ukiwa fundi mzuri wa magari makubwa au madogo na ukatangiliza uaminifu, hautolala njaa.

3- Ukiwa fundi mzuri wa kuchomelea vyuma na ukiwa muaminifu, hautolala njaa.

4- Ukiwa fundi ujenzi mzuri na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

5- Ukiwa dereva wa bajaji/bodaboda na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

Zaidi nasisitiza vijana kuweka aibu kando na wasiwe wavivu huu mwaka 2023 wasisubiri kazi za degree zao.

Hayo ni kwauchache, naomba kuwasilisha...🙏
Jifunze kushona vijora vya mamakimbo hautalala njaa na utaajiri wakukusaidia, vijora hushonwa kwa timu huwa havishonwi kwa mtu mmojammoja.
 
Ukiwa kwenye sector ya Usafirishaji uwe Konda, Dereva Bajaj, Bodaboda, Daladala as long as inahusisha abiria Nakuhakikishia 2023 is going to be your Year! Usisahau Key point :UAMINIFU
sio unakuwa Bodaboda unapigiwa Simu unaulizwa uko wapi unasema upo jirani kumbe Upo Km 20 away unafata abiria mwingine na Unasisitiza unakuja! Hii tabia inakera na inapoteza Wateja!
TAMAA na UONGO vikupite kushoto
 
Tupeane tips wakuu, jinsi ya kuingia 2023 kwa focus zaidi katika kutengeneza pesa kupitia ujuzi (skills) ambao hauhitaji uwe na degree wala masters.
Kidijitali ukijua vizuri kucharaza proposals kwenye freelancing platform hulali njaa, ukipatia digital marketing, ila mostly ukiwa na gadgets kali kama simu na pc + kifurushi hulali njaa ng'o mwisho ukikomalia financial markets imeisha
 
1- Ukipika chakula kizuri na ukazingatia usafi, hautolala njaa.

2- Ukiwa fundi mzuri wa magari makubwa au madogo na ukatangiliza uaminifu, hautolala njaa.

3- Ukiwa fundi mzuri wa kuchomelea vyuma na ukiwa muaminifu, hautolala njaa.

4- Ukiwa fundi ujenzi mzuri na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

5- Ukiwa dereva wa bajaji/bodaboda na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

6- Vijana jifunzeni hata kusuka/kunyoa hamtokosa pesa ya kula.

Zaidi nasisitiza vijana kuweka aibu kando na wasiwe wavivu huu mwaka 2023 wasisubiri kazi za degree zao.

Hayo ni kwauchache, naomba kuwasilisha...[emoji120]
Brother na useremala pia. Hii haikulazi njaa hata kidogo, haiitaji uwe na utaalamu sana, uwe unajua kushika nyundo, kukata kwa msumeno, kupiga msasa , hivyo tu hailali na njaa wakati wowote.

Mfano wakati fulani binafsi nilikua sina ishu kabisa, nikabeba nyundo na msumeno na futi, nikaenda sokoni, yaani kwenye masoko makubwa haya, huko nilipata kazi za kurekebisha meza meza na banda mpaka nilivyokuja kukaa sawa nilikua na kiasi kikubwa sana cha hela, na connection nyingi sana nilipata huko.
 
Kuna sehemu zinahitaji nguvu kazi kama hivi
JamiiForums-1660967584.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1- Ukipika chakula kizuri na ukazingatia usafi, hautolala njaa.

2- Ukiwa fundi mzuri wa magari makubwa au madogo na ukatangiliza uaminifu, hautolala njaa.

3- Ukiwa fundi mzuri wa kuchomelea vyuma na ukiwa muaminifu, hautolala njaa.

4- Ukiwa fundi ujenzi mzuri na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

5- Ukiwa dereva wa bajaji/bodaboda na ukawa muaminifu, hautolala njaa.

6- Vijana jifunzeni hata kusuka/kunyoa hamtokosa pesa ya kula.

Zaidi nasisitiza vijana kuweka aibu kando na wasiwe wavivu huu mwaka 2023 wasisubiri kazi za degree zao.

Hayo ni kwauchache, naomba kuwasilisha...🙏
Bila kuathiri ibara ya 5 na weka namba yako ya Simu ya kiswaswadu, usikose na smartphone Kwa ajili ya wateja wanaopenda kutumia Whatsapp. Iwe na chaji Muda wote. Ukiamua usibebe abiria mwingine yyt uwena wateja wako tu. Inawezekana pia.

Safari za mbezi, posts, tegeta, mbagala hutakosa 10k Kwa safari moja.

Utaepukana na kuporwa pikipiki au Bajaji. Utakuwa kama Uber vile.

Lkn acha ulevi wa pombe, Malaya , bangi nk
 
Nimekukubali sana, hongera kwa kulitambua hilo naamini sasa utakuwa mwalimu mzuri kwa wengne ambao wanaamini upigaji ndo ujanja, kiufupi upigaji sio ujanja ila ni maandalizi ya kuifanya kesho yako kuwa ngumu zaidi ya leo
Nina msubiri mjinga mmoja aliwe kichwa na Allah, mjinga huyu anajiona malumalu. Yaani nimekaa naomba Mungu ampe anachostahili
 
Mchezaji wa mpira..
Hasa mchangani(ndondo),popote pale chochote kile kikubwa pana uwanja wa mpira hulali njaa..

NB/UWE MPAMBANAJI
Kama una kipaji kwenye ndondo unatretiwa kama king. Sema anasa ni adui wa maendeleo ya Mwanaume.
 
Back
Top Bottom