1- Ukipika chakula kizuri na ukazingatia usafi, hautolala njaa.
2- Ukiwa fundi mzuri wa magari makubwa au madogo na ukatangiliza uaminifu, hautolala njaa.
3- Ukiwa fundi mzuri wa kuchomelea vyuma na ukiwa muaminifu, hautolala njaa.
4- Ukiwa fundi ujenzi mzuri na ukawa muaminifu, hautolala njaa.
5- Ukiwa dereva wa bajaji/bodaboda na ukawa muaminifu, hautolala njaa.
6- Vijana jifunzeni hata kusuka/kunyoa hamtokosa pesa ya kula.
Zaidi nasisitiza vijana kuweka aibu kando na wasiwe wavivu huu mwaka 2023 wasisubiri kazi za degree zao.
Hayo ni kwauchache, naomba kuwasilisha...[emoji120]