Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Undava King

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2017
Posts
3,422
Reaction score
5,659
Jana nilipata wasaha wa kutizama luninga na bahati nzuri nikabahatika kutupia jicho katika muvi zetu almaarufu Bongo movies, kusema ukweli vijana wanajitahidi na kufanya kila wawezalo kuweza kuifikisha sanaa yao mbali licha ya changamoto kibao.

Baadhi ya changamoto kuu za kiwanda hiki ni;

1. Elimu - Taaluma nchini haijatambua bado sanaa na mwamko wa vyuo na michepuo yake haitoi nafasi katika sanaa.

2. Wasanii wachache mno wenye elimu ya sanaa na wengi huigiza au kuongoza filamu kwa uzoefu na hamasa tu.

3. Exposure - Kutokana na ukata uliopo wasanii wetu hawawezi kujifunza kwa njia ya tembea uone mengi.

Uwekezaji duni, kukosa haki na fursa sawa kama nchi zingine katika mauzo, udhibiti, usambazaji na matangazo, Kukosa kupewa kipaumbele, mazingira duni ya kuigizia,n.k.

Pamoja na yote haya watu hawa wanaendelea kila siku kuandika hadithi, kubuni na kuwekeza kidogo walichonacho kuhakikisha sisi na familia zetu tunaburudika na kuelimika.

Ila kilichonishangaza zaidi ni pale nilipobaini kuwa kuna kukwama kwingine kwa sanaa kunakochagizwa na kile ninachoweza kukiita ulimbukeni wa serikali katika kuielewa sanaa.

Hivi ni kipi kilipelekea maamuzi ya kusitisha/marufuku kwa wasanii wanapoigiza uhusika wa kipolisi au kijeshi wasivae sare za jeshi letu?

Ikumbukwe India na Korea ambao ni mifano ya mataifa machache yaliyopiga hatua katika soko la filamu na tunaongoza kutizama na kuzisifia muvi zao za kiintelijensia almaarufu detective, wanajitangaza kupitia filamu hizo duniani kote.

Nchi za wenzetu hawaoni taabu kuwaunga mkono wasanii wao linapokuja suala la kuitangaza nchi, msanii atapewa ushirikiano wa mafunzo, difenda, ambulance, zimamoto, kituo cha polisi, polisi halisi wachache akihitaji wakuigizia, sare mpaka na silaha zikihitajika katika sanaa yake ili mradi anachofanya ni kuigiza na pia kwa maslahi mapana ya kuelimisha jamii na uchumi wa taifa lake.

Sasa leo hii bongo muvi ukiitizama unabaki kushangaa tu, mtu anayeitwa polisi na vile alivyo-appear katika uhusika ni vituko.

Tukihitaji sanaa yetu ikue basi tuwaache wasanii wawe na fikra huru na mipaka ya shughuli zao isiingiliwe na hisia binafsi au mihemko ya kundi fulani katika jamii kuguswa na kazi ya fasihi.

Kama ilivyoshuhudiwa juzi kati wauguzi wa afya wakidai wasiigizwe, hii haina utofauti na polisi ambao nao baada ya kutizama igizo la filamu iliyochezwa na waigizaji wakongwe almaarufu J Plus na Seba walikataa sare zao zisitumike tena kisa kwa hisia zao binafsi walijihisi kudhalilishwa.

Badala yake tuipe sanaa nguvu yake ili iweze kui-shape jamii katika mwelekeo chanya pasipo na vizuizi mwisho wa siku sanaa kama kazi nyingine rasmi inahitajika kumnufaisha msanii na taifa pia.

Kwani kwa kutokufanya hivyo na tukiendelea na hiki kinachofanya sanaa yetu iendelee kukosa uhai na uhalisia wake tunakuwa tumezalisha yafuatayo;

Sanaa inakosa uthubutu, ubunifu, uhalisia na uhuru wa mitizamo tofauti.

Nchi inakosa fursa ya kujitangaza vyema kupitia sanaa na inazidi kuua vipaji na kupunguza ajira kwa vijana wake.
 
Uko sahihi. Kungekuwepo na utaratibi wa kutoa vibali maalum kwa wasanii wetu kufanyia maigizo yao. Changamoto kubwa hatuna vyuo bora vya kuzalisha waigizaji wa viwango vya kimataifa.

Kwa nchi kama Tanzania, ukiwa binti mrembo mwenye sura nzuri, makalio makubwa! Au kijana mwrnye muonekana wa kuvutia; ndiyo hutumika kama sifa ya kuwa msanii wa Bongo muvi
.
 
Uko sahihi. Kungekuwepo na utaratibi wa kutoa vibali maalum kwa wasanii wetu kufanyia maigizo yao. Changamoto kubwa hatuna vyuo bora vya kuzalisha waigizaji wa viwango vya kimataifa.

Kwa nchi kama Tanzania, ukiwa binti mrembo mwenye sura nzuri, makalio makubwa! Au kijana mwrnye muonekana wa kuvutia; ndiyo hutumika kama sifa ya kuwa msanii wa Bongo muvi
.
Ni kweli maana nchi imeipa sanaa mgongo hamna mchango wowote ule wa serikali, wadau wala taasisi za elimu katika kuendeleza na kuboresha sanaa badala yake tunategemea ikuwe yenyewe baadae tujisifie kuwa bongo movies ni juhudi zetu.
 
Ni kero kweli hao majamaa kujiona wao katika nchi hii ni chombo ambacho akiwezi hata kuigizwa na raia wake kwa kuwa wao ndiyo dola, hii si sawa katika nchi ya kidemokrasia.
Kwa Nchi zilizoendelea
Scenes zote zinazohusisha mambo ya usalama, huwa wana usalama wanakuwepo kucoach wahusika.

Magari ya Polisi yanakuwepo kwa uhalisia wake.


Tatizo la Tanzania ni soko bado halijakaa sawa,wasanii hawafaidiki na utengenezaji wa filamu sababu ya uharamia
 
Kuna kipindi wakati nipo Arusha kuna wasanii walitaka igiza movie ya kivita walikataliwa kata kata....
Nchi hii bado ipo nyuma sana katika mambo mengi, hapo mamlaka husika ziliamini waigizaji wenda wanamalengo ya kuwajengea wananchi wao fikra za uasi, haya ni mawazo ya kijima yaliyopitwa na wakati hivi sasa dunia ni kijiji wakati unamfungia mwigizaji wako asipige hatua wengine upande wa pili wanazidi kuuza za kwao na kukugeuza dampo la filamu zao.
 
Tatizo wanatumia hizo uniform kuteflect hali halisi ya jeshi letu...i.e waonevu, ubabe kwa wanyonge, respect kwa wenye pesa na Rushwa... hakuna anaetaka kutangazwa negatively. Anyway nakumbuka Penzi la misukosuko yule jamaa aliyeigiza Ins. J Plus angependezea sana na uzi...bahati mbaya ni moja ya movie zangu za mwisho kuangalia Bongo Movie sijapata tena interest na hawa watu especially baada ya soko kuwa flooded na series kali za nje ilihali humu ndani tukaendelea kutoa vitu kwa mazoea.
 
Bongo movie na wenyewe wajiongeza bana, unakuta mtu anawaza au kutembea dakika 5 nzima bila kuwa na tukio la maana.
Hii yote ni kwa kuwa kiwanda hiki kinaendeshwa na watu unprofessional wengi na hakuna madirector wa maana, uandishi shallow wa script, waigizaji wachanga (katika uelewa wa filamu), low motivation, teknolojia duni, maslahi madogo n.k vyote hivi uchangia ubora hafifu wa filamu zetu kuweza kuvutia watazamaji au kushindana sokoni na movies zingine kutoka barani asia na amerika.
 
Tatizo wanatumia hizo uniform kuteflect hali halisi ya jeshi letu...i.e waonevu, ubabe kwa wanyonge, respect kwa wenye pesa na Rushwa... hakuna anaetaka kutangazwa negatively. Anyway nakumbuka Penzi la misukosuko yule jamaa aliyeigiza Ins. J Plus angependezea sana na uzi...bahati mbaya ni moja ya movie zangu za mwisho kuangalia Bongo Movie sijapata tena interest na hawa watu especially baada ya soko kuwa flooded na series kali za nje ilihali humu ndani tukaendelea kutoa vitu kwa mazoea.
Majeshi mengi duniani yanafanya ukatili na uonevu kwa raia wake lakini hicho si kigezo cha kuibana sanaa isiwaumbe katika kazi zao, kwani sanaa haipo kumfurahisha mtu bali kuibua yale yaliyopo katika jamii na kufunza au kuadilisha umma.

Kazi ya sanaa ya uigizaji ni sawa na kazi ya sanaa zingine kama uandishi wa habari, uchoraji, muziki n.k haijalishi ujumbe wao umekugusa kiasi gani ni dhambi kuwapangia wasanii hawa namna unavyotaka sanaa yao ikuguse kisa unayo mamlaka fulani ya kuweza kuwaziba midomo.

Bongo muvi mwanzoni ilianza kwa stahili ya kuvutia tena kama ingepata mwendelezo ingekuwa giant kuliko bongo fleva na kututangaza duniani kote lakini kwa kuwa tuna serikali isiyoona fursa katika sanaa isipokuwa uitumia sanaa kujipatia followers tu ilipuuziwa na tukajikuta tunavutiwa na akina prince jumong na prison break za wale walioamua kuipa nafasi sanaa katika nchi zao.
 
Kwa Nchi zilizoendelea
Scenes zote zinazohusisha mambo ya usalama, huwa wana usalama wanakuwepo kucoach wahusika.

Magari ya Polisi yanakuwepo kwa uhalisia wake.


Tatizo la Tanzania ni soko bado halijakaa sawa,wasanii hawafaidiki na utengenezaji wa filamu sababu ya uharamia

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app

Huko kote hatuwezi kulifikisha soko letu hili la filamu ikiwa serikali haitoi ushirikiano wa kutosha na kutimiza majukumu yake ipasavyo katika sekta hii.

Sanaa ni biashara na kama biashara zote zilivyo zinahitaji sera nzuri,usimamizi madhubuti, miundombinu, uwekezaji katika rasilimali watu, fedha na bidhaa
ambapo kama nchi tunalo soko kubwa la watazamaji wa filamu zetu la ndani na nje ya nchi tena tunaweza vuka mpaka mipaka ya bara la afrika tukaliteka soko la huko arabuni na sehemu zingine duniani.

Kingine ukiachilia mbali mchango wa serikali kunahitajika juhudi za sekta binafsi kuiona sanaa kwa jicho lingine kuwa ni fursa pia wawekeze katika soko hili ambalo ni kubwa mno ila limetekelezwa, badala ya kujazana kwenye biashara haramu za kamari na bahati nasibu.
 
Hili mbona linawezekana na ni rahisi sana. Tatizo vijana wahuni sana hawachelewi kutumia hizo uniform kutapeli watu.
 
Back
Top Bottom