Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Kuna kipindi wakati nipo Arusha kuna wasanii walitaka igiza movie ya kivita walikataliwa kata kata....
Hiyo vita ingetengenezwaje na zile bunduki za watoto zinazowasha vitaa taa huku zinatoa milio kama gari la Azam ice cream na vinyimbo nyimbo mixer kisauti kinasema "Tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu" [emoji444][emoji445][emoji444][emoji445][emoji444][emoji444][emoji445][emoji444]
 
Kwa Nchi zilizoendelea
Scenes zote zinazohusisha mambo ya usalama, huwa wana usalama wanakuwepo kucoach wahusika.

Magari ya Polisi yanakuwepo kwa uhalisia wake.

Tatizo la Tanzania ni soko bado halijakaa sawa,wasanii hawafaidiki na utengenezaji wa filamu sababu ya uharamia
Hapo hapo usisahau swala la bajeti kuwa finyu kitu ambacho kinachochea dharau hata kwa mamlaka wakiona wanaona hampo serious. Mnafanya maigizo badala ya kutengeneza filamu.
 
Hiyo vita ingetengenezwaje na zile bunduki za watoto zinazowasha vitaa taa huku zinatoa milio kama gari la Azam ice cream na vinyimbo nyimbo mixer kisauti kinasema "Tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu" [emoji444][emoji445][emoji444][emoji445][emoji444][emoji444][emoji445][emoji444]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Hili mbona linawezekana na ni rahisi sana. Tatizo vijana wahuni sana hawachelewi kutumia hizo uniform kutapeli watu.
Kwani hizo sare unapewa kama zawadi ukauzie sura mpaka utapeli watu?
 
Wasanii hawajui kuwa kifungu cha 178 cha Sheria ya kanuni ya makosa ya jinai inatoa ruhusa kuvaa nguo za jeshi ikiwa utapata ruksa kutoka kwa IGP, au kwa Rais.
Pia wasanii au wapanda stejini wanaruhusiwa kuvaa hayo mavazi wakiwa majukwaani tuu

Changamoto Wanajeshi na Polisi wetu pia ni wavivu kusoma.
 
Hiyo vita ingetengenezwaje na zile bunduki za watoto zinazowasha vitaa taa huku zinatoa milio kama gari la Azam ice cream na vinyimbo nyimbo mixer kisauti kinasema "Tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu" [emoji444][emoji445][emoji444][emoji445][emoji444][emoji444][emoji445][emoji444]
Hahahaaa umenikumbusha wakati watoto wangu wakiwa wadogo daah sijavisikia siku nyungi
 
Hili mbona linawezekana na ni rahisi sana. Tatizo vijana wahuni sana hawachelewi kutumia hizo uniform kutapeli watu.
Naunga mkono hoja 100%.
Zaidi vijana hawajitambui na kuzingatia Taratibu. Utamkuta msanii anaweka nafasi ya Askari JWTZ halafu hafuati taratibu za kupata kibali cha kutumia uniform(Wanafahamu kabisa hairuhusiwi kisheria raia kuvaa sare za jeshi lolote hapa Tz bila Uhalali) lakini wanakimbilia kutoa majibu rahisi "Tumenyimwa" ukimwuliza umenyimwa kivipi? anajibu kirahisi-rahisi tu "Ah! sijui bhana hawa majamaa hawataki eti tutumie sare zao......." Yani vijana dah! wanarahisisha kila kitu (nadhani including hata kitu cha hatari). Halafu hawatafuti Ushauri na Uzoefu kwa waliowatangulia i.e. Wazee-wabobezi katika Tasnia hiyo.
Mm naona: 1. Ipo haja ya kuwapatia mafunzo ya Taratibu zihusuzo Tasnia hii, miiko yake na Utambuzi wa jukumu lao Muhimu la kuielimisha jamii. Wajue kwamba Hiyo sio Starehe kwao kama waigizaji. Ni ajira; ni Ofisi. Anaestarehe ni yule mwanajamii Mtazamaji.
2. Kabla ya kutoa(Relese) Igizo lao, wafanye pilot study kama kweli linakidhi Lengo (theme) la Igizo hilo na kama linaonekana katika Uhalisia wake. Maigizo yao mengi kwa mfano mtu mwanaume analia hovyo kitu ambacho kiuhalisia katika jamii haiko hivyo. Kitu wanachokipatia vizuri ni ile make-up katika igizo husika.
 
Hiyo vita ingetengenezwaje na zile bunduki za watoto zinazowasha vitaa taa huku zinatoa milio kama gari la Azam ice cream na vinyimbo nyimbo mixer kisauti kinasema "Tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu tai yai yaaaaah nyichachachachuuuuuu" [emoji444][emoji445][emoji444][emoji445][emoji444][emoji444][emoji445][emoji444]
Igizo la kivita linahitaji uwekezaji(In puts) mkubwa. Linahitaji Watu wengi na Mdhamini, Vitendea kazi(e.g.Bunduki/Silaha na magari-vita), Eneo au mandhari maalum e.g. mapori/vijijini) na Muda mwingi pia Fedha halisi Uwezeshaji(Malipo kwa waigizaji n.k.). Wasanii wetu sidhani kama watakuwa na Uwezo huo.
 
Wasanii hawajui kuwa kifungu cha 178 cha Sheria ya kanuni ya makosa ya jinai inatoa ruhusa kuvaa nguo za jeshi ikiwa utapata ruksa kutoka kwa IGP, au kwa Rais.
Pia wasanii au wapanda stejini wanaruhusiwa kuvaa hayo mavazi wakiwa majukwaani tuu

Changamoto Wanajeshi na Polisi wetu pia ni wavivu kusoma.
Dah kama ndizo sheria tulizonazo basi ni ngumu mno kufanikisha jambo hilo kwa sababu ikiwa kila inapotakiwa kufanyika shughuli yeyote ya sanaa inayohusisha kutumia sare za jeshi lolote lile la Tanzania mpaka uwasiliane na Amiri jeshi mkuu au IGP mbona ni shughuli nzito.

Pili umesema kuwa msanii anapokuwa akiperform anaruhusiwa kuvaa sare ila akishuka stejini anapaswa kuvua kama ni hivyo basi haina tofauti na anayeigiza kwa maana anapokuwa kwenye filamu ni muda wake wa performance na kama ulichosema ni sahihi basi wana haki ya kuigiza wakiwa wamevalia rasmi kama askari ila nje ya igizo hawaruhusiwi kuwa na vitu hivyo wala kuonekana wakivitumia pasipo ruhusa ya Rais.
 
Igizo la kivita linahitaji uwekezaji(In puts) mkubwa. Linahitaji Watu wengi na Mdhamini, Vitendea kazi(e.g.Bunduki/Silaha na magari-vita), Eneo au mandhari maalum e.g. mapori/vijijini) na Muda mwingi pia Fedha halisi Uwezeshaji(Malipo kwa waigizaji n.k.). Wasanii wetu sidhani kama watakuwa na Uwezo huo.
Ndiyo maana kunahitajika mchango wa wadau na serikali katika kulifanikisha hilo.

Mfano mzuri nchi kama Korea, India au Amerika wamefikia hatua hadi ya kutenga maeneo na miji ijulikane kama maeneo ya sanaa.

Wanawekeza kwenye kuwajengea uwezo wasanii wao na waongozaji wa filamu lakini pia kuwahakikishia masoko na kudhibiti ubora wa filamu zao na kuhakikisha wanafanya wawezalo kutangaza tamaduni, biashara, vivutio na lugha zao kupitia sanaa zao.

Miaka ya zamani tuliijua Marekani kupitia muvi zake za 'kikomando' na India muvi zake za 'kipolisi', huku Nigeria 'Uchawi', china 'kungfu', Thailand 'Thai boxing' na ufilipino 'mapenzi' baadae ikaongezeka Korea ikabobea kwenye stori za ufalme na upelelezi.

Lakini ikumbukwe kuwa Tanzania hatukuwa nyuma nyakati hizo tulikuwa tumeanza kuigiza tena muvi kali kabisa za kikomando mfano "Shamba Kubwa" hii ni muvi ambayo watoto wa mwaka 2000s hawawezi kuijua.

Bongo movies ya kizazi kipya ilianza na filamu yake ya kwanza ya Monalisa na TID- "Girlfriend" kama sikosei na baada ya hapo ikatokea kupendwa sana na watazamaji hata kabla ya filamu za nje kuanza kufurika nchini lakini mwamko wa kuipa support ukakosekana na kupelekea mpaka wa leo hatuna mafanikio mazuri katika kiwanda hiki.

Tanzania ni moja ya nchi yenye vijana wenye vipaji vya mapigano na masumbwi kuliko nchi yeyote inayocheza filamu za namna hiyo Afrika lakini kinachotuangusha ni uwekezaji mdogo katika filamu, hatuna teknolojia, vifaa duni, kukosa mafunzo, mazingira magumu ya kuigizia, bajeti ndogo,n.k

Pili upande wa maujanja, kukopi haraka na mazingira, nakuenda na wakati tunaongoza Afrika kinachotuponza sisi ni umasikini lahiti kama wasanii wetu wangeliwezeshwa japo kidogo tungeliteka soko la Afrika na kuwapita Nigeria, SA na Ghana tena kwa kasi ya 5G.
 
Ulimbukeni mkubwa. Halafu inawaharibia maana watu wanavaa marapurapu eti ndiyo polisi.
Yaani ukimwangalia polisi kavaa kiraia na suruali lake la kitambaa la kipaimara na ana mimic maneno ya kimazoea "Aroo afande Mwita" na sentro yake ni fremu ya duka unabaki tu kuvumilia hiyo scene ipite na ukiwa na rimoti mkononi unajikuta mara moja ushashawishika kubadili channel.
 
Jana nilipata wasaha wa kutizama luninga na bahati nzuri nikabahatika kutupia jicho katika muvi zetu almaarufu Bongo movies, kusema ukweli vijana wanajitahidi na kufanya kila wawezalo kuweza kuifikisha sanaa yao mbali licha ya changamoto kibao.

Baadhi ya changamoto kuu za kiwanda hiki ni;

1. Elimu - Taaluma nchini haijatambua bado sanaa na mwamko wa vyuo na michepuo yake haitoi nafasi katika sanaa.

2. Wasanii wachache mno wenye elimu ya sanaa na wengi huigiza au kuongoza filamu kwa uzoefu na hamasa tu.

3. Exposure - Kutokana na ukata uliopo wasanii wetu hawawezi kujifunza kwa njia ya tembea uone mengi.

Uwekezaji duni, kukosa haki na fursa sawa kama nchi zingine katika mauzo, udhibiti, usambazaji na matangazo, Kukosa kupewa kipaumbele, mazingira duni ya kuigizia,n.k.

Pamoja na yote haya watu hawa wanaendelea kila siku kuandika hadithi, kubuni na kuwekeza kidogo walichonacho kuhakikisha sisi na familia zetu tunaburudika na kuelimika.

Ila kilichonishangaza zaidi ni pale nilipobaini kuwa kuna kukwama kwingine kwa sanaa kunakochagizwa na kile ninachoweza kukiita ulimbukeni wa serikali katika kuielewa sanaa.

Hivi ni kipi kilipelekea maamuzi ya kusitisha/marufuku kwa wasanii wanapoigiza uhusika wa kipolisi au kijeshi wasivae sare za jeshi letu?

Ikumbukwe India na Korea ambao ni mifano ya mataifa machache yaliyopiga hatua katika soko la filamu na tunaongoza kutizama na kuzisifia muvi zao za kiintelijensia almaarufu detective, wanajitangaza kupitia filamu hizo duniani kote.

Nchi za wenzetu hawaoni taabu kuwaunga mkono wasanii wao linapokuja suala la kuitangaza nchi, msanii atapewa ushirikiano wa mafunzo, difenda, ambulance, zimamoto, kituo cha polisi, polisi halisi wachache akihitaji wakuigizia, sare mpaka na silaha zikihitajika katika sanaa yake ili mradi anachofanya ni kuigiza na pia kwa maslahi mapana ya kuelimisha jamii na uchumi wa taifa lake.

Sasa leo hii bongo muvi ukiitizama unabaki kushangaa tu, mtu anayeitwa polisi na vile alivyo-appear katika uhusika ni vituko.

Tukihitaji sanaa yetu ikue basi tuwaache wasanii wawe na fikra huru na mipaka ya shughuli zao isiingiliwe na hisia binafsi au mihemko ya kundi fulani katika jamii kuguswa na kazi ya fasihi.

Kama ilivyoshuhudiwa juzi kati wauguzi wa afya wakidai wasiigizwe, hii haina utofauti na polisi ambao nao baada ya kutizama igizo la filamu iliyochezwa na waigizaji wakongwe almaarufu J Plus na Seba walikataa sare zao zisitumike tena kisa kwa hisia zao binafsi walijihisi kudhalilishwa.

Badala yake tuipe sanaa nguvu yake ili iweze kui-shape jamii katika mwelekeo chanya pasipo na vizuizi mwisho wa siku sanaa kama kazi nyingine rasmi inahitajika kumnufaisha msanii na taifa pia.

Kwani kwa kutokufanya hivyo na tukiendelea na hiki kinachofanya sanaa yetu iendelee kukosa uhai na uhalisia wake tunakuwa tumezalisha yafuatayo;

Sanaa inakosa uthubutu, ubunifu, uhalisia na uhuru wa mitizamo tofauti.

Nchi inakosa fursa ya kujitangaza vyema kupitia sanaa na inazidi kuua vipaji na kupunguza ajira kwa vijana wake.
Yeyote asiyetaka kuigizwa, ni kuhofia uduni wa huduma zao kuwekwa hadharani.
 
Dah kama ndizo sheria tulizonazo basi ni ngumu mno kufanikisha jambo hilo kwa sababu ikiwa kila inapotakiwa kufanyika shughuli yeyote ya sanaa inayohusisha kutumia sare za jeshi lolote lile la Tanzania mpaka uwasiliane na Amiri jeshi mkuu au IGP mbona ni shughuli nzito.

Pili umesema kuwa msanii anapokuwa akiperform anaruhusiwa kuvaa sare ila akishuka stejini anapaswa kuvua kama ni hivyo basi haina tofauti na anayeigiza kwa maana anapokuwa kwenye filamu ni muda wake wa performance na kama ulichosema ni sahihi basi wana haki ya kuigiza wakiwa wamevalia rasmi kama askari ila nje ya igizo hawaruhusiwi kuwa na vitu hivyo wala kuonekana wakivitumia pasipo ruhusa ya Rais.
Sasa utashangaa unaweza kuwa stejini na umevaa nguo za jwtz na eti wakaja kukuvua au ukishuka wanakuwashia moto!!
Kumbe shida ni hao hawasomi.

Kuhusu kupata kibali ni rahisi tuu.
 
Attachments

  • Screenshot_20230322-071745.png
    Screenshot_20230322-071745.png
    45.1 KB · Views: 4
Ndiyo maana kunahitajika mchango wa wadau na serikali katika kulifanikisha hilo.

Mfano mzuri nchi kama Korea, India au Amerika wamefikia hatua hadi ya kutenga maeneo na miji ijulikane kama maeneo ya sanaa.

Wanawekeza kwenye kuwajengea uwezo wasanii wao na waongozaji wa filamu lakini pia kuwahakikishia masoko na kudhibiti ubora wa filamu zao na kuhakikisha wanafanya wawezalo kutangaza tamaduni, biashara, vivutio na lugha zao kupitia sanaa zao.

Miaka ya zamani tuliijua Marekani kupitia muvi zake za 'kikomando' na India muvi zake za 'kipolisi', huku Nigeria 'Uchawi', china 'kungfu', Thailand 'Thai boxing' na ufilipino 'mapenzi' baadae ikaongezeka Korea ikabobea kwenye stori za ufalme na upelelezi.

Lakini ikumbukwe kuwa Tanzania hatukuwa nyuma nyakati hizo tulikuwa tumeanza kuigiza tena muvi kali kabisa za kikomando mfano "Shamba Kubwa" hii ni muvi ambayo watoto wa mwaka 2000s hawawezi kuijua.

Bongo movies ya kizazi kipya ilianza na filamu yake ya kwanza ya Monalisa na TID- "Girlfriend" kama sikosei na baada ya hapo ikatokea kupendwa sana na watazamaji hata kabla ya filamu za nje kuanza kufurika nchini lakini mwamko wa kuipa support ukakosekana na kupelekea mpaka wa leo hatuna mafanikio mazuri katika kiwanda hiki.

Tanzania ni moja ya nchi yenye vijana wenye vipaji vya mapigano na masumbwi kuliko nchi yeyote inayocheza filamu za namna hiyo Afrika lakini kinachotuangusha ni uwekezaji mdogo katika filamu, hatuna teknolojia, vifaa duni, kukosa mafunzo, mazingira magumu ya kuigizia, bajeti ndogo,n.k

Pili upande wa maujanja, kukopi haraka na mazingira, nakuenda na wakati tunaongoza Afrika kinachotuponza sisi ni umasikini lahiti kama wasanii wetu wangeliwezeshwa japo kidogo tungeliteka soko la Afrika na kuwapita Nigeria, SA na Ghana tena kwa kasi ya 5G.
Nanukuu: Tanzania ni moja ya nchi yenye vijana wenye vipaji vya mapigano na masumbwi kuliko nchi yeyote inayocheza filamu za namna hiyo Afrika lakini kinachotuangusha ni uwekezaji mdogo katika filamu, hatuna teknolojia, vifaa duni, kukosa mafunzo, mazingira magumu ya kuigizia, bajeti ndogo,n.k Mwisho wa kunukuu.
Hii 👆 👆 👆 ndio changamoto kubwa na pia kuwekewa vikwazo visivyo vya lazima e.g. upatikanaji wa Sare (Uniform) stahiki katika maigizo au hata kuazimwa vifaa/vitendea kazi maalum ili kufanikisha scenario fulani katika igizo.
Wawekezaji e.g. wale wenye uwezo kifedha (Matajiri)hawaja wezeshwa kuona kwamba hiyo Tasnia nayo ni mojawapo ya fursa ya Uwekezaji. Naamini wakihamasishwa watathubutu kujipa roho ya Ujasiriamali katika Tasnia hii.
Serikali inao wajibu mkubwa wa kuwalinda na kuzilinda kazi zao kwa kutoa Hati miliki kuliko ilivyo sasa hivi vijana mpaka huku vijijini wananakili nyimbo,video na kufanya biashara katika vibanda kwa kutumuia Laptops na Flash bila hata kuwapa chochote waliohenyeka kutengeneza filamu hizo.
 
Pia nahis kuna tatizo kwenye sheria zetu,sijawai kuona movie iliyotengenezwa na maproducers wakubwa kutumia mandhari ya kibongo (labda serengeti NP) vinginevyo wanaitumia Kenya zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom