Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ni ulimbukeni kuwazuia wasanii kutumia mavazi ya Polisi katika filamu zao

Ndiyo matokeo yake kwa sababu ukitoka nje ya hapo ni mtafutano mwishowe sanaa inakosa maana na kudhoofisha soko lake.
Yaani na mbilinge mbilinge za siasa lakini hamna filamu inayohusiana na siasa.

Na umaarufu alionao mwl. Nyerere lakini hamna hata filamu yake hata moja.
 
Jana nilipata wasaha wa kutizama luninga na bahati nzuri nikabahatika kutupia jicho katika muvi zetu almaarufu Bongo movies, kusema ukweli vijana wanajitahidi na kufanya kila wawezalo kuweza kuifikisha sanaa yao mbali licha ya changamoto kibao.

Baadhi ya changamoto kuu za kiwanda hiki ni;

1. Elimu - Taaluma nchini haijatambua bado sanaa na mwamko wa vyuo na michepuo yake haitoi nafasi katika sanaa.

2. Wasanii wachache mno wenye elimu ya sanaa na wengi huigiza au kuongoza filamu kwa uzoefu na hamasa tu.

3. Exposure - Kutokana na ukata uliopo wasanii wetu hawawezi kujifunza kwa njia ya tembea uone mengi.

Uwekezaji duni, kukosa haki na fursa sawa kama nchi zingine katika mauzo, udhibiti, usambazaji na matangazo, Kukosa kupewa kipaumbele, mazingira duni ya kuigizia,n.k.

Pamoja na yote haya watu hawa wanaendelea kila siku kuandika hadithi, kubuni na kuwekeza kidogo walichonacho kuhakikisha sisi na familia zetu tunaburudika na kuelimika.

Ila kilichonishangaza zaidi ni pale nilipobaini kuwa kuna kukwama kwingine kwa sanaa kunakochagizwa na kile ninachoweza kukiita ulimbukeni wa serikali katika kuielewa sanaa.

Hivi ni kipi kilipelekea maamuzi ya kusitisha/marufuku kwa wasanii wanapoigiza uhusika wa kipolisi au kijeshi wasivae sare za jeshi letu?

Ikumbukwe India na Korea ambao ni mifano ya mataifa machache yaliyopiga hatua katika soko la filamu na tunaongoza kutizama na kuzisifia muvi zao za kiintelijensia almaarufu detective, wanajitangaza kupitia filamu hizo duniani kote.

Nchi za wenzetu hawaoni taabu kuwaunga mkono wasanii wao linapokuja suala la kuitangaza nchi, msanii atapewa ushirikiano wa mafunzo, difenda, ambulance, zimamoto, kituo cha polisi, polisi halisi wachache akihitaji wakuigizia, sare mpaka na silaha zikihitajika katika sanaa yake ili mradi anachofanya ni kuigiza na pia kwa maslahi mapana ya kuelimisha jamii na uchumi wa taifa lake.

Sasa leo hii bongo muvi ukiitizama unabaki kushangaa tu, mtu anayeitwa polisi na vile alivyo-appear katika uhusika ni vituko.

Tukihitaji sanaa yetu ikue basi tuwaache wasanii wawe na fikra huru na mipaka ya shughuli zao isiingiliwe na hisia binafsi au mihemko ya kundi fulani katika jamii kuguswa na kazi ya fasihi.

Kama ilivyoshuhudiwa juzi kati wauguzi wa afya wakidai wasiigizwe, hii haina utofauti na polisi ambao nao baada ya kutizama igizo la filamu iliyochezwa na waigizaji wakongwe almaarufu J Plus na Seba walikataa sare zao zisitumike tena kisa kwa hisia zao binafsi walijihisi kudhalilishwa.

Badala yake tuipe sanaa nguvu yake ili iweze kui-shape jamii katika mwelekeo chanya pasipo na vizuizi mwisho wa siku sanaa kama kazi nyingine rasmi inahitajika kumnufaisha msanii na taifa pia.

Kwani kwa kutokufanya hivyo na tukiendelea na hiki kinachofanya sanaa yetu iendelee kukosa uhai na uhalisia wake tunakuwa tumezalisha yafuatayo;

Sanaa inakosa uthubutu, ubunifu, uhalisia na uhuru wa mitizamo tofauti.

Nchi inakosa fursa ya kujitangaza vyema kupitia sanaa na inazidi kuua vipaji na kupunguza ajira kwa vijana wake.
Video ya Amazangu ama zao ya East Coast team ilifungiwa kutokana na wasanii kuvaa mavazi ya kijeshi, japo ilikuwa ni video bora sana kwa kipindi kile.
 
Yaani na mbilinge mbilinge za siasa lakini hamna filamu inayohusiana na siasa.

Na umaarufu alionao mwl. Nyerere lakini hamna hata filamu yake hata moja.
Siyo nyerere tu hakina Mkwawa, Mirambo, chief songea wa majimaji n.k kiufupi nchi kama Korea kusini zimekula pesa ndefu sana na kutangaza historia ya nchi yao duniani pote kupitia muvi za kifalme almaarufu muvi za vijijini pale serikali yao ilipotambua umuhimu wa kuwekeza na kuipa support ya kutosha tasnia ya filamu.
 
Video ya Amazangu ama zao ya East Coast team ilifungiwa kutokana na wasanii kuvaa mavazi ya kijeshi, japo ilikuwa ni video bora sana kwa kipindi kile.
Hivi kumbe video hii pia ilifungiwa?
Umenikumbusha kisa cha sande mjeda kupokea kichapo na kuvuliwa nguo hadharani na kisa cha kina Roma na Stamina kushindwa kushoot video ya wimbo wao nchini Kenya na sare za jeshi kama alivyofanya mwenzao Khaligraph Jones kisa kuofia kufungiwa na kushtakiwa nchini mwao Tz.
 
Back
Top Bottom