karonga
JF-Expert Member
- Mar 19, 2017
- 777
- 1,280
Kuna changamoto kubwa Sana kwa mtu mzima kuumia au kuteswa na mpenzi, labda alichelewa kuanza mahusiano au changamoto za Kimaisha au kiafya, mimi binafsi kutokana na kujihusisha na mapenzj mapema, nimepitia mishale mingi Sana kiasi ambacho kwa Sasa haiwezekani tena kuumizwa na mpenzi, nishawahi kuumizwa huko ninakotoka, lakini baada ya hapo sikuwahi kuyachukulia mapenzi very serious, au tuseme kwenye mapenzi sijawahi kurukwa na akili nikazama mazima kwa demu, huwa nashangaa Sana watu wakiumizwa na mapenzi wengine wana collapse mazima, hawawezi kuinuka tena, wanabaki maisha Yao yote na visasi visivyoisha, ilimradi vurugu tupu, kwa upande wako unatoa ushauri gani kwa watu wazima labda miaka 30 na kuendelea, ambao wamezama kimapenzi na hawawezi kujinasua?