Ni uongo Kudai 80% Walikataa Mfumo wa Vyama Vingi

Swali rahisi tu unakatika mauno kibao.

Swali ni hili, ni lini Tanzania tulipiga kura za maoni? Fullstop.
acha matusi tafadhali. kama ni matusi fungua uzi wa matusi tutukanane. besides huu uzi hukuufungua wewe. Jifunze kuwa na adabu. Hukuzaliwa ili uwe mtukanaji. jifunze kustahi wazazi waliokuzaa wakitumaini kuwa utakuwa mstaarabu.

Kura ya maoni ilipigwa nchi nzima ikisimamiwa na jopo lenye hadhiya kijaji chini ya jaji kisanga kwa mbali jaji mkuu nyalali kama mwangalizi mkuu. Bila shaka kwa umri wako hata akina jaji nyalali huwajui.
 
Kwa wakati ule wajinga
Walikuwa wengi zaidi ukilinganisha Na sasa ingawa kwa sasa wajinga bando wapo wengi lakini uelewa kidogo umeanza kuonekana ijapokuwa bado.
 
Walitembea nchi nzima,na kila eneo kulitengwa vituo vya kutolea maoni. Nafikili kama sikosei tume ile iliongozwa na mhe jaji kisanga,au mhe sherukindo.
Swali linabaki palepale, ni lini Watanzania walipiga kura za maoni kukataa au kukubali mfumo wa vyama vingi?

Ccm haiukutaka kabisa vyama vingi na ndio maana ilipiga marufuku vyama vingi, vyama vingi vilikuwepo kabla Ccm msidhani watu ni machizi.

Ccm imeruhusu vyama vingi kwa mbinyo wa IFM na world bank na kwakuwa pesa zao wañazitaka na Nyerere alikuwa na vision kubwa ya kuona mbele kifuatacho yeye ndio akashinikiza Ccm ikubali mfumo wa vyama vingi, hakukuwa na namna na ndio maana katiba mpaka leo ni ya Chama kimoja.
 
Kwa wakati ule wajinga
Walikuwa wengi zaidi ukilinganisha Na sasa ingawa kwa sasa wajinga bando wapo wengi lakini uelewa kidogo umeanza kuonekana ijapokuwa bado.
Watu wengi mpo gizani ndio maana wajinga.

Vyama vingi vilikuwepo kabla ya Ccm, na mgombea binafsi alikuwepo pia lakini mpaka leo Ccm wanabinya haki ya mgombea binafsi.
 
20% ndiyo walisema hawataki
 
Sidhani kama umri wa mleta uzi huu, unaweza kubadilisha ukweli aliouandika!
Hakuna kura iliyopigwa kuulizia suala hilo. Kama kuulizana, labda waliulizana makada waliokuwepo wakati huo!
Tume ya jaji nyalali
 
Watu wangapi walipiga kura?
 
Zamani matawi ya Ccm yalikuwa yanaitwa zone, yalikuwa na sifa za Police post, ukikamatwa na mgambo unawekwa lockup kwenye zone ya Ccm kabla ya kupelekwa kituo kikuu cha Polisi.
 
Matola,soma andiko lako halafu ujitafakali,unakubali kipi na unakataa kipi?. Mpk mda huu hoja yako iliyokuwa imenyooka umeiharibu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…