Ni uongo Kudai 80% Walikataa Mfumo wa Vyama Vingi

Pascal Mayalla ulikuwepo enzi hizo thibitisha hili.

Ni kweli 'multiparty' ilikuja kwa shinikizo la wakubwa wa dunia hilo halina ubishi.
Kwanza ni kweli mfumo wa vyama vingi ulikuja kwa shinikizo la mabeberu!. Ilipigwa kura unayoitwa white paper, watu waliulizwa kama wanataka mfumo wa vyama vingi au tuendelee na mfumo wa chama kimoja, Asilimia 80% wakataka tuendelee na chama kimoja.

p
 
Unajuwa kwa nini Gabon wanajeshi wamefuta uchaguzi na kuchukuwa Madaraka?
 
Watu wangapi walipiga hiyo kura??
 
Akikujibu nishtue[emoji1787]
Nyie watoto wa juzi kaeni kimya sisi baba zenu tunapojadili mambo yaliyotokea kabla hamjazaliwa.

Usidhani mimi ni mtoto mwenzako. Nilimvisha skafu Mwalimu Nyerere alipotembelea Iringa. Nikiwa JKT, Operesheni miaka 25 ya JKT nilienda kujenga nyumba ya Rais Mstaafu Mwalimu Nyerere.

Ndiye niliyeandaa risala ya kumuaga afande CDF Musuguri, alipostaafu.
 
Bila shaka umezaliwa baada ya mwaka 1991. Au mwaka 1990-91 wakati michakato hiyo inafanyika ulikuwa bado unanyonya.

Tatizo ninyi vitoto vya juzi ambavyo hamkushuhudia chochote, na wala hampendi kufuatilia mambo, mmejawa uwongo na ushabiki wa kipuuzi.

Tuliokuwepo wakati huo, tunakueleza kilichotokea. Chukua haya ninayokueleza kama ukweli unaofundishwa kwako mtoto wa juzi.

Hakukuwahi kuwa na kura yoyote ya wananchi kuamua kama wanataka mfumo wa vyama vingi au hapana. Mambo yaliishia kwenye vikao vya chama. Utambue wakati huo CCM ilikuwa kama mahakama ja ilikuwa juu ya Serikali. Ni wakati mke akigombezwa na mumewe, atamweleza mumewe, 'naenda kukushtaki CCM', na mume ananywea kwa kuogopa kupelekwa ofusi ya CCM.
 
Kwa nini umeamua kuwa mwongo kiasi hiki? Nilikuwepo wakati huo, nikiwa kijana kabisa, na nikiwa na cheo ndani ya UVCCM. Hakuna kura iliyopigwa, usiwadanganye watu ambao walikuwa bado hawajazaliwa.
 
Watu wangapi walipiga kura?
nenda mahakamu kuu. record zipo
povu lote hili la nini? kwa hiyo unataka siasa ya vyama vingi tz ifutwe?
 
Sijui unamanisha nn? Wajinga kwa maana ipi?



Kutokujua faida za kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi kuwa ni nyingi sana kuliko kwenye chama kimoja.

Political awareness ni ndogo sana.

Hata sasa ratio ya wenye ufahamu ni ndogo sana ukilinganisha na wajinga.
 
Sijui unamanisha nn? Wajinga kwa maana ipi?



Kutokujua faida za kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi kuliko chama kimoja.

Political awareness ni ndogo sana.

Hata sasa ratio ya wenye ufahamu ni ndogo sana ukilinganisha na wajinga.
 
nadhani kipindi hicho watu wengi walikuwa hawajui umuhimu wa vyama vingi ila serikali ilibidi ikubali mfumo wa vyama vingi kutokana na masharti ya wahisani.
 
Mwambie au mkumbushe mwaka 90 na 91 kulikuwa na tukio gani la kitaifa kuhusiana na mfumo wa vyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…