Ni uongo upi usio na mantiki umewahi kutana nao kwenye Bongo Movie?

Tunajenga kwa pesa zetu by Mwendazake
 
Si mpenzi sana wa Bongo movies ila sometimes kuna mazingira huwa inatokea naangalia bila kupenda (mf; kwenye mabasi ya mikoani)

Huwa napenda sana kusoma subtitles za kingereza, kiukweli zina makosa mengi ya grammar na typing errors. Hapo ndo wanajinasibu wanataka waende kimataifa.! Bado tunasafari ndefu sana
 
Kamera ya kijinga Kama mark 3 ambayo hutumika na bongo movie nyingi unakodi kwa 50 kwa siku,lakini hata hivyo ulisema ukimbie nayo kumfuata muigizaju picha itacheza,hapa utahitaji gumbo,ambayo ni ghali,au dolly,ni ghali pia..bongo movie wanaungaunga hawana mitaji,so ngoma inabidi ipigwe chapu ili kupunguza gharama
 
Ndoto yangu siku moja kuwa na studio kubwa ya kutayarisha filamu (nina mpango wa kusomea ) ambayo italeta mapinduzi makubwa bongo movie.

Si zungumzii studio kama marvel huko mbali na pagumu Sana kufikia ,lkn kastudio flani ambacho kitazalisha movie zenye quality za kimataifa
 
Watakuja kina ray kwa kujiona masuper star watataka uwatengenezee bure ili wakutangaze.
 
Watakuja kina ray kwa kujiona masuper star watataka uwatengenezee bure ili wakutangaze.
Kama nipo hatua za mwanzo nitakubali (sio free kabisa) hili kutengeneza brand ,lkn nikashapata jina nitaaza kuwa expensive na Mimi and there will be nothing Free
 
Kama nipo hatua za mwanzo nitakubali (sio free kabisa) hili kutengeneza brand ,lkn nikashapata jina nitaaza kuwa expensive na Mimi and there will be nothing Free
Hata kama watatayarisha movie zao zenye uongo ndani yake!!? [emoji1][emoji1]
Kweli, aliye juu atabaki juu!!
Matokeo yake hako ka Studio kako hakatokuwa na maana tena ya mapinduzi!!
 
Mbona huzungumzii ile ,muandaji ,ray, muandishi,ray, directer ,rey, steling ,rey, yaani mtu mmoja anakuwa ameshiriki sehemu kibaaao hii pia inachangia sana kuaribu
 
Mbona huzungumzii ile ,muandaji ,ray, muandishi,ray, directer ,rey, steling ,rey, yaani mtu mmoja anakuwa ameshiriki sehemu kibaaao hii pia inachangia sana kuaribu
Hapo bado hujamzungumzia Tin White, anashiriki kila sekta, lakini kiuharisia unakuta ni photographer wa mabibo, tena mpiga picha za studio ndo anafanya mambo!!
Nchi hii ni ngumu sana! filamu za wenzetu zinaandaliwa na zaidi ya kampuni tatu! utakuta Syfy, Netflix humo humo, ma mabilioni ya pesa! na charachters wa kutosha!!
 
Kuonja sumu Kama imekolea .
Jini kuvaa jezi ya Barcelona.
Ndani usiku nje Mchana .
kuongea na simu na mtu wa mkoa afu unamskia chumba Cha 2.
 
Mchawi kaingia ndani ili amnyonye damu msukule wake halafu akawasha taa vili amuone [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kafungwa miaka 30 jela kwa kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi! alivyomaliza kifungo wanaonesha mwanae analingana naye! Pia baba wa kijana aliyefungwa anakuja kumpokea akiwa amevaa nguo zilezile alizovaa miaka 30 iliyopita, kuanzia shati hadi viatu [emoji23][emoji23]
 
Huba imekosa reality. Matukio yamekosa ubunifu. In real life hayawezi kutokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…