Ni uongo upi usio na mantiki umewahi kutana nao kwenye Bongo Movie?

Ni uongo upi usio na mantiki umewahi kutana nao kwenye Bongo Movie?

Huba imekosa reality. Matukio yamekosa ubunifu. In real life hayawezi kutokea.
Nakasirika sana nikikuta home wanaangalia huo upuuzi na wanafahamu nikiingia tu wanabadili channel.
 
Si mpenzi sana wa Bongo movies ila sometimes kuna mazingira huwa inatokea naangalia bila kupenda (mf; kwenye mabasi ya mikoani)

Huwa napenda sana kusoma subtitles za kingereza, kiukweli zina makosa mengi ya grammar na typing errors. Hapo ndo wanajinasibu wanataka waende kimataifa.! Bado tunasafari ndefu sana
Mambo ya "You are going where?"
 
Mwanamke kutobadilisha mtindo wa nywele, yaani hata akikumbuka tukio la miaka 10 iliyopita msuko wake ni huo huo.

Mwanaume ndio usiseme, anaigiza anaishi maisha ya shida kijijini ila nywele zimewekwa wave, kachonga ndevu, kapaka black. kuanzia mwanzo wa movie hadi mwisho.

Kunq movie moja Hemedy anaigiza chizi ila nywele na ndevu zake hazikubadilika kuanzia kabla hajawa kichaa mpaka mwisho
 
Mawasiliano yako tafadhali tunahitaji watu kama nyie wenye mitazamo chanya ya kubaini matatizo na kwenda kuyatatua
 
Kwa upande wangu sio kila movie itakuwa na reality unayoitaka katika maisha ya kawaida mfano katika filam za wenzetu unakuta mtu anatoa moto 🔥 ambao kiukweli katika maisha ya kawaida haiwezekani yote hiyo ni njia ya kuwakilisha wazo na kufikisha ujumbe katika jamii
 
Back
Top Bottom