Ni upi Msimamo wa Serikali kuhusu Vipimo vinavyopima mwili mzima kwa Tsh. 20,000?

Ni upi Msimamo wa Serikali kuhusu Vipimo vinavyopima mwili mzima kwa Tsh. 20,000?

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Kuna kampeni kubwa inaendelea sehemu mbalimbali ambapo kuna wataalamu wanapita na kipimo cha kupima mwili mzima kwa 20,000.

Nina shauku ya kujua kutoka wizara ya Afya kuhusu msimamo wa serikali juu ya jambo hili.

Waziri Ummy, ikikupendeza tueleze.
 
Kuna kampeni kubwa inaendelea sehemu mbalimbali ambapo kuna wataalamu wanapita na kipimo cha kupima mwili mzima kwa 20,000.
Nina shauku ya kujua kutoka wizara ya Afya kuhusu msimamo wa serikali juu ya jambo hili.
Waziri Ummy,ikikupendeza tueleze.
Hakuna kipimo kinachopima mwili Mzima kwa mara moja Huo ni utapeli kama Utapeli mwingine tu
 
Acha uongo hajawahi kujibu swali hata moja, ni Gwajima pekee ndiyo huwa ana jibu, Ummy anakiburi, NHIF ipo hoi sababu ya uongozi mbovu wa Ummy. taja cha maana alichofanya Ummy pale Wizara ya Afya hata kimoja
Mkuu mbona uko na hasira sana?
Kumradhi nimechanganya madawa..kweli ni Gwajima...
Unaweza ua mtu
 
Nakumbuka kuna wachina fulani waliwahi kushikwa Buguruni wakiwa na mashine za namna hiyo na wao walienda mbali zaidi wakawa wanatibu (detoxification) kwa kuweka miguu kwenye mashine fulani then maji yanaanza kubadilika rangi wanakwambia "sumu" ndio inatoka hivyo. Sijui ile kesi iliishia wapi

Tanzania kwa nini baadhi yetu tunakosa maarifa?

Yaani kipimo cha mwili mzima 20,000... sidhani maana wapigaji wengi siku hizi bongo kwa kivuli cha bei nafuu..

Cheap is expensive
 
Back
Top Bottom