Pia pale mwenge mpakani karibu ya magorofa ya jeshi kuna sinagogi linaongozwa na mtu anajiita Nabii James Nyakia,huyu analaza watu kabisa sijui kama Wizara ya Afya imempa kibali hicho. Anadai mikono yake ina upako ina uwezo wa kufanya vipimo vya X-ray, Ultrasound, CT Scan, MRI na ghara ya kipimo ni Tsh.10,000/-. Anakuja kuwakamata kwenye tiba kwani wanapewa asali iliyowekwa kwenye kichupa kidogo cha ml 10 na bei yake inategemea na hali ya ukwasi wa mgonjwa lakini ni kati ya Tsh.50,000/- hadi Tsh. 350,000/- mwenyewe anaviita package.