Ni upi muda muafaka wa kuchumbiana?

Ni upi muda muafaka wa kuchumbiana?

Kajuni

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2009
Posts
483
Reaction score
186
Wadau poleni kwa majukumu. Bila kupoteza muda napenda kuwaomba ushauri wenu kuhusu muda muafaka wa wapenzi wawili kuwa katika uchumba.Nina umri wa miaka 27. Nipo katika kipindi kigumu mimi na mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano zaidi ya miaka miwili na nusu. Wazazi wetu wanatambua mahusiano yetu kwa kipindi chote hiki. Mwezi uliopita nilipata fursa ya kwenda kujitamulisha kwa wakwe zetu. Yatokanayo na utambulisho huo wazazi walikubaliana kwamba hakuna tatizo lolote ila inatakiwa tukae miaka mitatu zaidi ili kufahamiana zaidi. Je ushauri huo ni sawa? ni kipindi gani watu hukaa katika uchumba?? au kuna ajenda ya siri ili tuweze kuachana? au wazazi hawajapenda mie na huyo mchumba wangu tuonane?
 
Samahani mkuu, naomba nikuulize. Tukuambie karibu JF au tukuulize ulikuwa wapi siku zote?

Kajuni
Junior Member
Join Date : 27th May 2009
Posts : 3
Thanks
0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power : 0
 
Wadau poleni kwa majukumu. Bila kupoteza muda napenda kuwaomba ushauri wenu kuhusu muda muafaka wa wapenzi wawili kuwa katika uchumba.Nina umri wa miaka 27. Nipo katika kipindi kigumu mimi na mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano zaidi ya miaka miwili na nusu. Wazazi wetu wanatambua mahusiano yetu kwa kipindi chote hiki. Mwezi uliopita nilipata fursa ya kwenda kujitamulisha kwa wakwe zetu. Yatokanayo na utambulisho huo wazazi walikubaliana kwamba hakuna tatizo lolote ila inatakiwa tukae miaka mitatu zaidi ili kufahamiana zaidi. Je ushauri huo ni sawa? ni kipindi gani watu hukaa katika uchumba?? au kuna ajenda ya siri ili tuweze kuachana? au wazazi hawajapenda mie na huyo mchumba wangu tuonane?

When you are 1 month old
 
Hivi unatakiwa ufahamiane na wakwe miaka hiyo mitatu ya ziada au nani hasa??
Waulize kwanini ukae miaka mitatu zaidi wakati ulishakaa miaka nae miaka miwili zaidi??
Waulize bila woga kwamba unatakiwa ufahamu kitu gani zaidi ambacho hujakifahamu miaka miwili na huyo mwanamke??
 
zamani kuepuka mizengwe kama hii watu walikuwa wanajazana mimba kwanza!labda na wewe utumie mbinu hii:wink2:
 
Sipiyuuuuuuu? yaani umeingia kwenye mtego mkuu? Can't you smell N4G?
 
zamani kuepuka mizengwe kama hii watu walikuwa wanajazana mimba kwanza!labda na wewe utumie mbinu hii:wink2:

we unamshauri mwenzio apachikwe mimba? duh atarudi tena hapa kuomba ushauri ooh nimezaa nae ila wazazi wake hawanitaki mara anmimba yangu kwao wamenikataa. miaka 27 unaweza fanya maamuzi wewe na mpenzi wako...... kwanza wewe ni wa kike au kiume!
 
Ni nyie wawili kukubaliana wazazi ni kutoa baraka na miaka hiyo miwili nusu naamini mmekwisha fahamiana vya kutosha
 
Hiyo miaka mitatu unasubiri mke/mume au wazazi.
Halafu acha utoto bana we mkubwa sasa 27yrs?? Toa maamuzi yako si kungoja wazazi.
 
Miaka miwili duh kwa tamaduni zetu zanzibar tushapata watoto wawili hapo huna kizazi tena...kujuana munajuana katika ndoa, ushauri wangu ni kwamba hapo wazee wanachojabu kutaka kuona presha yako tu,ikiwa unataka leo basi hawapingiiii,ni makubalianao yenu na kwa maelezo yako wanaonekana wameshakubali suala....

Weka presha nduguuu..
 
sasa ufahamiane zaidi na nani? Huyo mchumba ndo unasema miaka 2 mnajuana..... Sasa na wazazi wake mjuane kivipi.....mbona haieleweki?
 
Nafikiri wazazi wapo sawa ingawa sioni umuhimu wa wao kuwapangia hadi muda wa kuchunguzana.
 
zamani kuepuka mizengwe kama hii watu walikuwa wanajazana mimba kwanza!labda na wewe utumie mbinu hii:wink2:
Ushauri huu anautoa Pauline!!!???
Jamii sasa kweli itakaa sawa....Ushauri huu angeutoa Paulo tungesema ni udhalilishaji wa kijinsia.
 
Kwa kifupi hao wazazi hawataki ww kuwa na binti yao, so uwaambie ukweli msimamo wako. Labda wanataka kutngsha kiberiti waonyeshe kuwa kimejaa
 
Wadau poleni kwa majukumu. Bila kupoteza muda napenda kuwaomba ushauri wenu kuhusu muda muafaka wa wapenzi wawili kuwa katika uchumba.Nina umri wa miaka 27. Nipo katika kipindi kigumu mimi na mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano zaidi ya miaka miwili na nusu. Wazazi wetu wanatambua mahusiano yetu kwa kipindi chote hiki. Mwezi uliopita nilipata fursa ya kwenda kujitamulisha kwa wakwe zetu. Yatokanayo na utambulisho huo wazazi walikubaliana kwamba hakuna tatizo lolote ila inatakiwa tukae miaka mitatu zaidi ili kufahamiana zaidi. Je ushauri huo ni sawa? ni kipindi gani watu hukaa katika uchumba?? au kuna ajenda ya siri ili tuweze kuachana? au wazazi hawajapenda mie na huyo mchumba wangu tuonane?

Hao ni wakwe wa ajabu sana cjapata kuona.
 
Mkuu
Nilisikia harufu lakin nikapuuzia
Ngoja ni FBI
Lakin huyu ni wa 2009

Mkuu huyo inaonekana alijipanga tangu longi. Thinking pattern is exact, the type of issues she presents are the same

we siku hizi ulipata kusikia wapi mtu anakwenda kujitambulisha anaambiwa wasubiri muda wote huo.
 
Hao wazazi labda wana sababu zao nyingine na sio kujuana. Uchumba wa miaka 5 sijui ni uchumba gani kwa sababu ushafikia umri ambao unaweza kuoa. Labda kama wazazi wanafikiria bado hamjawa tayari kuoana kwa kuwa kuna watu wana mitazamo kuwa kuoa mpaka mwanaume ufikishe miaka 30 (sio lazima kabisa). Pengine ungeweza kuwaambia kuwa mshajuana vya kutosha na mnataka muishi kama wenza kihalali badala ya kuiba. Ni vizuri kuheshimu wazazi lakini wasipokuwa wazi inakuwa ni tatizo kidogo. Na wewe usiwe mwoga kupita kiasi kuelezea hisia zako hata kama ni wazazi.
 
hao ni wakwe wa ajabu sana cjapata kuona.

hawatak waoane
ndo mana wamewapa miaka mitatu na wanajua mpk ikipita na wao watakuwa washaachana....hawajaafiki mpango wao.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom