Kajuni
JF-Expert Member
- May 27, 2009
- 483
- 186
Wadau poleni kwa majukumu. Bila kupoteza muda napenda kuwaomba ushauri wenu kuhusu muda muafaka wa wapenzi wawili kuwa katika uchumba.Nina umri wa miaka 27. Nipo katika kipindi kigumu mimi na mpenzi wangu ambaye tumekuwa katika mahusiano zaidi ya miaka miwili na nusu. Wazazi wetu wanatambua mahusiano yetu kwa kipindi chote hiki. Mwezi uliopita nilipata fursa ya kwenda kujitamulisha kwa wakwe zetu. Yatokanayo na utambulisho huo wazazi walikubaliana kwamba hakuna tatizo lolote ila inatakiwa tukae miaka mitatu zaidi ili kufahamiana zaidi. Je ushauri huo ni sawa? ni kipindi gani watu hukaa katika uchumba?? au kuna ajenda ya siri ili tuweze kuachana? au wazazi hawajapenda mie na huyo mchumba wangu tuonane?