Ni upi muda unaotakiwa kuoa tena ikiwa utafiwa na mke

Ni upi muda unaotakiwa kuoa tena ikiwa utafiwa na mke

Kafuta

Senior Member
Joined
Oct 15, 2010
Posts
119
Reaction score
29
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf
 
  • Thanks
Reactions: BAK
pole sana....unaweza kuoa tu
 
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf
Nadhani hapo red ulimaanisha Months!
Mkuu, ishu hii ni dependent on various factors.
Kwa utamaduni wangu haiwezekani kuoa kabla ya at least mwaka, yaani mpaka ujenge kaburi la marehemu na kukaa kwa muda wa ziada, which counts to approx 1.5 years!
Lakini pia mzigo alio nao aliyefiwa huangaliwa sana(kama ilivyo ishu yako)
Sijui kwa mila zenu wanaangalia nini!
 
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf
Pole sana mkuu. Machungu hayawezi kwisha kwa haraka hivyo, tulia kwanza usikimbilie kuoa, sina hakika kama hiyo itakuondolea machungu, wakati mwingine inaweza kukuongezea zaidi. Watoto ni wadogo, kama mama yupo mchukue akusaidie kulea watoto ili uendelee na shughuli zako. Au tafuta h'girl mtu mzima akusaidie kuangalia watoto. Kuoa bado ni mapema mno. Pole again na Mungu akutangulie.
 
Kama uikuwa na mpango wa kando wakati mkeo akiwa hai, fanya mpango umuoe huyo.
Kama hakuwepo ulikuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa mkeo, basi mwombe Mungu akupe nguvu kwanza.

Halafu akupe neema ya kupata mtu mzima mwenye akili timamu na ubinadamu awalee watoto wako.
Halafu baada ya hapo utaangalia ni kweli unahitaji kuoa kwa sababu ya watoto?

Manake unaweza kuoa ukidhani unawasaidia watoto kumbe ndo unawatesa watoto wako.
 
Take your time and have patience. Muhimu: Ukimpata wa kumwoa sisitiza awe na uhusiano mzuri na upendo wa dhati kwa watoto ulioachiwa nahofia ikiwa kinyume basi utakuwa umeongeza pilipili na chumvi kwenye maumivu.
Pole sana mkuu kwani kupoteza mtu unashare nae shelter na kitanda ni ngumu sana. Pole sana
 
Pole kaka angu kwa masahibu yaliyokukuta. nakushauri kaa mwenyewe lea watoto wako maana akija mama mwingine hapo hao watoto watakiona cha mtema kuni na kuishia kumkumbuka mama yao kila siku. Wanawake sisi wakati mwingine tuna roho mbaya sana. yaani utakuta mtu anadhibu watoto utadhani sio binadamu anasahau kama na yeye anaweza tangulia na wa kwake wakafanyiwa hivi. haya yapo na tunayaona mitaani kwetu. Pia unaweza kuoa ila inabidi uwe makini sana kwenye kuchagua mke wa kuweza kukaa na wanao kama wa kwake.
 
Pole sana ndugu,
Ingekuwa vyema zaidi kama ungesubiri at least 2yrs,
Waweza kutafuta dada wa kazi kwa ajili ya kucare wanao na shughuli zote za home,
Kumpata(mweza) atakaye walea wanao kama walivyo kuwa wakilelewa na mama yao hilo nalo zoezi jingine.
 
kwanza pole sana
Pili we unataka kuoa ajili gani??
unatafuta mtu wa kuwatunza watoto,
unatafuta mtu wa ku m replace mkeo au
wataka kuoa ajili umempata umpendae??

samahani sana kwa maswali yangu....
 
  • Thanks
Reactions: SMU
pole sana kwa matatizo mkuu.me nadhani muda wowote unafaa mradi ipite miezi japo nane hadi mwaka ili watu wasielewe tofauti.ila kwa matatizo kama ya kwako haitakiwi kufanya maamuzi ya kukurupuka usije ukajuta baadae.
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf
 
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf

Kaka Kafuta pole saana na kufiwa pia na majonzi ulonayo mana una mtihani mzito. Kuhusu kuoa tena, nimependa sana the way Paka Jimmy ameelezea.

Kitu ambacho wewe personally inabidi uzingatie ni kua ukitaka kuoa sababu tu upunguze machungu na kurahisisha majukumu ulonayo unaweza kuta umeruka majivu na kukanyaga moto. Saizi wewe ni baba wa watoto wawili ambao unalea mwenyewe ni tofauti na kama ungekua upo single, kum replace mkeo haitawezekana mana alikua mama yao wa dhati hivyo na mapenzi juu ya watoto yalikua hivyo hivyo.

Uangalie sana wanawake utakao kutana nao, na ukikutana nao alafu unatangaza kabisa unahitaji mke - wanawake wako desperate kuolewa, atajifanya mwema anapenda watoto na bla bla kibao. Nenda/Fanya taratibu hili suala; kua patient, muombe Mungu akupe nguvu za ziada na mwanamke atakae faa na angalia wanawake wanaokuzunguka na unaowafahamu vizuri. Jitahidi saana usioe mdada very young awe walau mature kidogo but before hujaamua msome kwanza acha kabisa kuwatangazia you want to marry, ikiwezekana wambie kabisa sitarajii....
 
pole kwa kufiwa muda utakapofika M/mungu atakupa my wife wako mpya na kuanza maisha mapya,2lia kama miezi kadhaa
 
Pole sana kwa kufiwa na mkeo (kipenzi). Sikubaliani na wewe kuhusu suala la kuoa kwa sababu ulizotoa. Kuoa kwa sababu yoyote ile nje ya love si kuoa. kama ni majukumu, tafuta housegirl au hata ndugu kijijini aje alee wanao. Watoto wa miaka nane si wadogo sana, wanaweza kukaa na housegirl. Tena ningekushauri uendelee kukaa single kwa muda zaidi watoto wakue. Nakwambia utaja oa hao watoto wapate shida kwani wanawake sisi tuna roho mbaya sana when it comes to husband's children. My dad and mom divorced when I was 13 and my young sister 10 but my loving dad hakuoa na hiyo imetufanya tuwe na bright future, tulilelewa na house maid kibibi. Our dady was so close to us telling us everything that we should and should not do including dating. Jenga ukaribu na wanao utaweza kuwalea tu.
 
Hata kama ulikuwa na nyumba ndogo, ihache iendelee kukupa service at a distance. Ukiipa promotion utaona mziki wake.
 
Kuna mtu alikuja na post kama hii bt hii yangu iko tofaut kidogo..she's r.i.p 8 mothr sasa,na aliacha watoto 2 wadogo miaka 6 na 10.kuwalea ni shughul coz wanasoma na jinsia yao tofaut.which way i can follow..ili niishi kama zaman..na machungu ni makali sana..naomba msaada wenu wana jf

Pole sana kwa msiba mkubwa. Watoto kuondokewa na mama yao wakiwa katika umri mdogo kama huo ni majonzi makubwa sana kwa Mume na Watoto na mara nyingi unaweza hata kulia kila ukiwaona watoto jinsi wanavyochanganyikiwa kumkosa mama yao na pia kumuulizia kama hawaelewi vizuri kilichotokea. Sijui kama kuna muda maalum wa kuamua kuoa tena.

Wengine wanaweza kuoa tena labda baada ya miaka miwili na wengine hata miaka 10 inaweza bado kuwawia vigumu kuoa tena kutokana na mapenzi makubwa yaliyopo kati ya Mume na marehemu mkewe na pia kuogopa labda mke mwingine anaweza asiwe anawatendea haki watoto walioachwa na marehemu.

Kwa maoni yangu huo ni uamuzi wako hasa baada ya kufuata mila na taratibu za kabila lako na pia kama mwenyewe unaona uko tayari kutafuta mwenzio ili uingie tena katika maisha ya ndoa. Pole sana na kila la heri.
 
kwanza pole sana
Pili we unataka kuoa ajili gani??
unatafuta mtu wa kuwatunza watoto,
unatafuta mtu wa ku m replace mkeo au
wataka kuoa ajili umempata umpendae??

samahani sana kwa maswali yangu....

sitaki kuoa kwa chochote kile.ilikua kwa ajir ya kujua ni muda gan unafaa kufanya hivyo.
 
kwanza pole sana
Pili we unataka kuoa ajili gani??
unatafuta mtu wa kuwatunza watoto,
unatafuta mtu wa ku m replace mkeo au
wataka kuoa ajili umempata umpendae??

samahani sana kwa maswali yangu....

Pole sana kwa kufiwa na mkeo (kipenzi). Sikubaliani na wewe kuhusu suala la kuoa kwa sababu ulizotoa. Kuoa kwa sababu yoyote ile nje ya love si kuoa. kama ni majukumu, tafuta housegirl au hata ndugu kijijini aje alee wanao. Watoto wa miaka nane si wadogo sana, wanaweza kukaa na housegirl. Tena ningekushauri uendelee kukaa single kwa muda zaidi watoto wakue. Nakwambia utaja oa hao watoto wapate shida kwani wanawake sisi tuna roho mbaya sana when it comes to husband's children. My dad and mom divorced when I was 13 and my young sister 10 but my loving dad hakuoa na hiyo imetufanya tuwe na bright future, tulilelewa na house maid kibibi. Our dady was so close to us telling us everything that we should and should not do including dating. Jenga ukaribu na wanao utaweza kuwalea tu.

Hata kama ulikuwa na nyumba ndogo, ihache iendelee kukupa service at a distance. Ukiipa promotion utaona mziki wake.

You two have spoken my mind. Thank you!
 
Kwanza niwashukurun kwa maneno na ushaur wenu mkubwa..mmesema sana.mmesema maneno ya busara..nimejifunza meng kutoka kwenu..cjaona mtu aliye sema vibaya..nimekubar sasa kua hapa jf ni mahal makini na ina watu makin..nasema nayabeba mliyonishaul na kuyafanyia kaz..kufiwa mke c mchezo ackwambie mtu.hasa kwa umri kama wetu wa miaka 31 hiv..tuombe mungu atupe kila lililo jema..asanten kwa mara nyingne.
 
Pole sana kwa msiba mkubwa.

Nakuombea Mungu akutie nguvu kwa kipindi hiki kigumu na kuwafariji wewe na watoto wako pia. Nafikiri mshirikishe Mungu zaidi katika suala hili la kuoa, ili ukimpata huyo mwingine aje awe mke mwema kwako na mama mzuri kwa watoto wako. Pole sana na Mungu akusaidie.
 
Pole sana Mkuu
Mungu awe pamoja nawe azidi kukutia nguvu
endelea kumtegemea Mungu
kuwa karibu na watoto waonyeshe upendo wa hali ya juu
usikimbilie kuoa kwa sasa subiri siku ikifika Mungu atakujalia
mke mwema mwenye upendo kwako na watoto wako

Back
Top Bottom