Mimi naomba niseme yafuatayo:
Sijui kama samaki hao wenye mwili wa binadamu juu na mkia wa samaki wapo kweli au la. Maana mimi binafsi sijawahi kuwaona. Ila kwa kipindi kirefu sasa nimekua nikifuatilia kwa ukaribu mambo haya yanayohusu dunia na hasa viumbe vya ajabu ajabu vinavyosadikiwa kuwepo au kuwahi kuwepo duniani pamoja na mambo mengine kama ya UFO n.k na nimegundua yafuatayo:
1. Habari za uwepo wa viumbe hawa hazijaanza jana wala juzi, na hazijaanzia sehemu moja. Watu mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani tangu enzi na enzi wameripoti kuwaona viumbe hawa, japo hakuna ushahidi yakinifu wa kudhibitisha hilo.
2. Taarifa za kisayansi zinasema kuwa, hadi sasa tumeweza kuikagua bahari kwa kiasi kisichozidi asilimia 10 - 20 tu. Kwa hiyo hatujui kwa uhakika ni kitu gani kinachoishi ndani ya asilimia takriban 80 ya bahari!
3. Kitu kimoja kinachonishangaza sana na kunitia wasiwasi ni kuwa, kila zinapotokea taarifa za kuonekana kwa viumbe wasioeleweka, au kuonekana kwa UFOs, nguvu kubwa sana imekua ikitumika kuficha taarifa hizo au inapotokea zikajulikana, nguvu kubwa sana hutumika kutangaza kwamba hicho kilichoonekana ni "feki"! Mfano ukiingia kwenye mitandao inayotoa taarifa hizi au hata youtube, utakuta juhudi kubwa zinafanyika ku declare kwamba habari /picha husika ni za uongo, ni za kughushi, ni za kutunga, ni photoshop n.k. bila ya kutoa ufafanuzi au kufanya uchunguzi wowote wa kina. Hii inatia wasi wasi kwamba pengine vitu hivi ni kweli ila kuna watu hawataki vijulikane.
4. Mwaka 2012 kituo kinachoaminika cha Animal Planet kilirusha kipindi kilicholenga kuwaaminisha watu kwamba samaki tajwa hapo juu wapo huku kikionyesha video na picha za samaki hao. Baada ya kuruka kwa kipindi hicho, Animal Planet walikuja kutangaza baadae kwamba video na picha zile walizorusha zilikua ni feki na hazina ukweli wowote! Hii kwangu naiona kama ni njia ya kitoto ya kuwafanya watu wapuuze habari zozote zitakazotolewa kuhusu viumbe hao kwa kisingizio kwamba "Hata Animal Planet walishawaonyesha na wakasema ni feki"!
5. Pengine unaweza kujiuliza: "Kama habari hizi ni za kweli, kwanini zisitangazwe tuu na vyombo vya habari? Kwanini zifanywe siri?" Ukweli ni kwamba kama itathibitika kwamba samaki hao wapo, hii itavuruga kabisa theory zilizopo kuanzia evolution, creation n.k na kusababisha maswali mengi ambayo hayatakua na majibu! Ndio maana nadhani habari nyingi zinazohusu UFOs, mermaids, giants, aliens n.k zinafanywa siri kubwa..
6. Kuna theory inaitwa "Acquatic Ape Theory" itafute uisome
7. Hapa duniani kuna mambo mengi sana ambayo tunadanganywa! Kuanzia historia ya dunia, ramani ya dunia, gravity, mbalamwezi, sayari, teknolojia, evolution, siasa, dini, na mengine mengi.. sitashangaa kama na hili ni mojawapo