Ni upi ukweli kuhusu Nguva (Samaki mtu)?

Kuna simulizi za ajabu ajabu kuhusu huyu samaki; kwa mfano wanasema kwamba mvuvi akimvua lazima kwanza afanye naye tendo la ndoa kama tambiko.

ni hadithi za mapokeo tu hakuna kitu hicho.ila katika hivo visa vya ajabu kuhusu huyu nguva inasemekana mvuvi aliydmvua nguva alilishwa yamini ili kuhakikisha hafanyi nae tendo la ndoa kwa vile nyama yake watu waliuziwa wakala?!
 


Nguva ni samaki ambayo anaishi kwenye maeneo ya tropiki. kuna aina nyingi kama dugagong ambaye umbile lake ni kama tembo kidogo na manatee ambaye ni huyo hapo juu. samaki hawa ni mamalia yaani huzaa kama binadamu au ng'ombe ila huzaa ndani ya maji na mara tu baada ya kuzaa humsukuma mwanawe juu ili aweze kuvuta hewa. samaki huyu hunyonyesha.
kuhusu mermaid ni hadithi za kale ambapo wasafiri wa enzi hizo hasa wa kaskazini wakati wakisafiri maeneo ya tropiki walivyowaona ndipo hadithi ya kuwa samaki nusu mtu ilipoanza na ikatiwa sukari sana mpaka dunia ya kaskazini waliamini kuwa kiumbe wa namna huyo yupo katika bahari za tropiki lakini siyo kweli.
 
Kiuhalisia nguva si samaki ila yuko katika kundi la wanyama kama walivyo tembo, nyati na wanyma wengine wanaonyonyesha. Ni story tu hizo zinasimuliwa kuhusu huyo nguva.
 
Duh, Baadae ulimfanyia nini? Kitoweo?
 
Nimejua kwamba kwa kimombo anaitwa mermaid bali ukweli kuhusu uwepo wake sijapata jibu bado
 
Kiuhalisia nguva si samaki ila yuko katika kundi la wanyama kama walivyo tembo, nyati na wanyma wengine wanaonyonyesha. Ni story tu hizo zinasimuliwa kuhusu huyo nguva.
Mbona hujaongeza binadam??? au siyo mnyama???
 
kama hakuna kitu kama hicho jamani mbona anasemwa sana? watu watoa wapi habari
zake?
Inaelekea wewe ni mtu wa bara ndiyo maana huamini lakini uliza watu wa pwani hasa wavuvi au wale wanaoishi maeneo ya visiwani au mwambao watakwambia. kuna watu wanakula samaki huyu ili mimi siwezi kabisa[ingawa ni mtu wa mwambao]
 
yupo....nilishawahi kumuona kwa macho yangu.....
bibie Preta punguza fix. ulimwona wapi ??? kwa taarifa tu , hakuna japo picha halisi ya Nguva uliyowapigwa hapa duniani. zoe za kutengeneza tu
 
Last edited by a moderator:
pia mara chache wakati ananyonyesha hupenda kuweka mkia chini , kichwa juu na kumkumbatia mtoto huku ana swing kama mtu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…