Ni upuuzi kufikiria kumuondoa Kocha Nabi

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Kwangu mimi Yanga kama timu tumejitahidi kwa kiasi kikubwa kufanya vizuri chini ya kocha Nabi kwa takriban msimu mwingine tena na kiukweli tutazidi kuimarika kadri timu inavyoendelea kuwa pamoja

Cha msingi tuone mapungufu yetu na kuyafanyia kazi lakini kama timu tupo vizuri na tutazidi kuwa bora
Tumwache kocha Nabi afanye kazi yake.

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Kocha yupo vizuri sawa,ila sisi,mashabiki wa nchi hii bila kujali ni simba au yanga Matamanio yetu ni ushindi daima siyo ndani tu mpk nje ya nchi.Ndo maana hata mchezaji wa club fulani akiitwa Timu yake ya Taifa tunamfuatilia na kutaka acheze na afunge.Kiu ya mashabiki wa nchi hii ni kubwa sana na uvumilivu ni mdogo. Ukiwa falsafa yako ni unbeaten iwe hivyo mpk nje siyo hapa hapa kwa ihefu au mbuni fc.
 
Nabi wa kazi gani sasa,ana wachezaji wazuri lakini mbinu hana ni lazima Yanga tufanye maamuzi magumu.makocha wapo wengi yeye sio wa kwanza,ebo!
 
Tatizo la Nabi kila inapotokea yanga inacheza na timu iliyopaki basi na kushambulia kwa pasi ndefu ni dhahama kwa yanga. Nabi anatakiwa awe na mbinu mbadala anapokutana na hali hiyo.
 
Ni chokochoko za mikia lia lia wa pale Msimbazi
 
Malengo ya Yanga siyo kuishia kumfunga Simba au timu nyingine za ndani. Yanga walifanya usajili mzuri kiasi cha kuweza kufanya vizuri hata mashindano ya kimataifa. Nabi ameonyesha kwa vitendo kuwa hana uwezo wala mbinu za kushinda game za kimataifa. Akishindwa kuingia hatua ya makundi kombe la Shirikisho, asepe aje kocha mwingine.
 
Na vipi atakayekuja akishindwa hata kutwaa ubingwa wa nbc ligi?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Facts
 
Ukishayaweka yakweka bayana malengo na matarajio ya usajili na gharama nyingine zilizotumika mpaka sasa kwaajili ya msimu huu, utapata jibu la either aachwe au akatafute changamoto sehemu nyingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukisema uwe na kocha ati achukue ubingwa wa afrika kwa viwango vyetu vya soka east/central africa basi utafukuza heta makocha mia

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Na nia yao tumuondoe tubaki bila kocha kama wao
We kocha ana zaidi ya michezo 42 bila kufungwa eti leo unaona hafai..ni wivu tu wa simba

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
mbona mnapenda kujifariji nyie viumbe?

kwa hiyo game za vipers, zesco &wale wanaijeria waliowapiga nje ndani hakuwa PROF. NABI?

Na kama ligi kuu NBC ingelikuwa na marefa bora na wenye kuzingatia sheria & kanuni huu wimbo wa unbeaten msingekuwa mnauimba popote.

Ukweli ni kwamba viongozi wa Yanga wanajua jinsi wanavyoshinda michezo na siyo kocha Nabi.
 
Kumbe MAKOLOKOLO siku hizi ni mbuni FC? [emoji1]
 
Tunakuaga na matarajio makubwa uku uwezo mdogo.Mpira wetu ni wakawaida sana unakuzwa na kuongea kwetu sana kuliko uhalisia.Bado hatuna mpira mkubwa kiasi chakuona makocha ni tatizo.Makocha wanajitahidi kwaviwango vyao kulingana na aina ya kikosi wanavyokua navyo ila sio kwamba timu zetu zina vikosi vipana kiasi chakushangaa yanga kufungwa na al hilal.Kinachotusumbua kikubwa ni kukosa uvumilivu na ujuaji.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nabi wa kazi gani sasa,ana wachezaji wazuri lakini mbinu hana ni lazima Yanga tufanye maamuzi magumu.makocha wapo wengi yeye sio wa kwanza,ebo!
MAKOLO sahauni kuhusu huyo Kocha, tumeshawajua mnajificha kwenye kichaka ili asiendelee kuwapa dozi ya kichapo kwenye mishono [emoji1787]
 
Kati ya yanga na hiyo al hilal ni nani anakikosi ghali?.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…