Ni usiku gani uliisha mapema kwako? Wangu huu hapa

Ni usiku gani uliisha mapema kwako? Wangu huu hapa

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,385
Reaction score
10,659
Nakumbuka mwaka 2001, nikiwa Morogoro, nilipata dili la matikiti Dar. Kuna mteja alihitaji matikiti 500, kila moja buku. Sasa mie nikayasaka nikapata kwa mia nne na muuzaji alikuwa na tikiti ka 800. Sasa issue ilikuwa nina Tsh 60,000 mfukoni. Nikaamua kwenda kwa rafiki yangu Nsindi. Huyu jamaa alikuwa na bucha na yeye ni mwenyeji wa Gamasala Tarime.

Sasa jamaa ni mkorofi haswa na wengi walimwogopa ila mie tulielewana japo kwa manati. Nikamuomba aniazime laki nne na nusu na nitamrudishia asubuhi. Jamaa nikamuelezea dili lenyewe na kumsihi sana aniazime. Akakubali ila kwa sharti kesho 12 asubuhi ataifuata ili akanunue ng'ombe machinjioni. Nilitoka hapo nduki na baiskeli kuelekea kwa mkulima wa matikiti.

Tobaaa, nilipofika, mkulima akaniambia kayauza yote kwa 450, nilimaindi ila nikaamua kurudisha pesa ya Mkurya. Heee, ile kujikagua nikakuta mfukoni kuna coin ya shilingi 20 tu! Nilivurugika. Nilizitafuta hizo jela mpaka kwenye Ndala nilizovaa.

Sasa Usiku huo, sikulala kabisa, nikawazaaa namwambiaje jamaa. Nilistuka saa 11 alfajili nagongewa mlango na sauti ya mkurya.

Je, wewe ni tukio gani lilikufanya usilale?
 
Nakumbuka mwaka 2001, nikiwa Morogoro, nilipata dili la matikiti Dar. Kuna mteja alihitaji matikiti 500, kila moja buku. Sasa mie nikayasaka nikapata kwa mia nne na muuzaji alikuwa na tikiti ka 800. Sasa issue ilikuwa nna Tsh 60,000 mfukoni. Nikaamua kwenda kwa rafiki yangu Nsindi. Huyu jamaa alikuwa na bucha na yeye ni mwenyeji wa Gamasala Tarime.

Sasa jamaa ni mkorofi haswa na wengi walimwogopa ila mie tulielewana japo kwa manati. Nikamuomba aniazime laki nne na nusu na nitamrudishia asubuhi. Jamaa nikamuelezea dili lenyewe na kumsihi Sana aniazime. Akakubali ila kwa sharti kesho 12 asubuhi ataifuata ili akanunue ng'ombe machinjioni. Nilitoka hapo nduki na baiskeli kuelekea kwa mkulima wa matikiti.

Tobaaa, nilipofika, mkulima akaniambia kayauza yote kwa 450, nilimaindi ila nikaamua kurudisha pesa ya mkurya. Heee, ile kujikagua nikakuta mfukoni kuna coin ya shilingi 20 tu!!! Nilivurugika. Nilizitafuta hizo jela mpaka kwenye Ndala nilizovaa...

Sasa Usiku huo, sikulala kabisa, nikawazaaa namwambiaje jamaa. Nilistuka saa 11 alfajili nagongewa mlango na sauti ya mkurya....

Je, wewe ni tukio gani lilikufanya usilale?
Sasa ukamwambiaje? Na hizi hela zilienda wap?
 
Nilipotuma SMS ya matusi kwa BOSS wangu bila kujua baadae napokea SMS kutoka kwa BOSS imeandikwa asante île kucheki sent item nakuta l'île tusi
Duuh! Cpati picha ulijinyenyekezajeee
 
Enzi nipo chuo kuna binti nilikuwa napiga mambo yetu sasa nikakosana nae usiku akanitumia meseji "kwanza nimeisha kuua kwa ukimwi" sikulala usiku kucha saa 11 nipo vct nacheki afya.
Haaaaa haaaaHaaaa uwiiiiiie utamu unaupenda lakini ukimwi hutaki
 
nimecheka hapo kuwa ulitafuta hela mpaka kwenye ndala dah hatri sasa mkuu hadi leo ujajua uliziangushia wapi??
 
Back
Top Bottom