Ni utapeli au napoteza bahati?

Huu ujinga mbona unafanyika mda mrefu sana
Na matapeli wako Kenya
Akutumie iphone sawa mkuu
 
yaani unajaa kizembe hasa..mzigo ufike baada ya masaa 9 alafuwakutafute mapema hivyo...namba uliyipigiwa nahisi si ya kenya ...na ungepiga video call wasingekuwa airport
 
Anakupa iphone 16 kwa kazi gani uliyofanya? Jiulize kwanza hilo swali
 
Ishanitokea mara nyingi hasa messenger hii ishu. Ukitaka kuwakomoa hawa waombe tracking number hapa ndio huwa wanapotelea hewani
 
Kuna watu wameshatepeliwa kwa staili hiyo hiyo. Waambie unataka kulipia wakupe account ya benki, ukiona wanang'ang'ania ulipe kwa simu watukane matusi yote
 
Ishanitokea mara nyingi hasa messenger hii ishu. Ukitaka kuwakomoa hawa waombe tracking number hapa ndio huwa wanapotelea hewani
Hta mimi sio huyo tu ila huyu ndo nilidumu nae kama miezi2 na wiki kadhaa. Swali langi connection na wabongo hutoa wapi maana kwa upande wa mzungu nilikuwa na uhakika100% kuwa ni kweli na kama ile no angetuma yeye direct nilikuwa nimeibwa asee. ila waliponicheki wabongo nikawa na mashaka mengi sana
 
Matapeli hao, achana nae. Nilishakuwa na rafiki nikaenda nae mpaka hatua ya kuniambia nitume kiasi ili nichangie mzigo kufika kupitia Nairobi.
 
waambie una kuja hapo Kenya, kuupokea mwenyewe [emoji23][emoji23].

Uki itwa kwenye fursa, jua wewe ndo fursa.
Ahahaha kuna mwanangu pia alishawahi kutana na hii akanishirikisha nikamuambia hawa matapeli utalia sio muda.

Anyway, ukikutana na suala kama hili ni simple, kwa kua mara nyingi hawa jamaa huwa ni wanaume ambao wanajifanya wanawake, we muombe umpigie video call muongee, hapa katu abadani hawezi kukubali kupigiwa video call.

Pili, omba atume location yake alipo kwa kupitia whatsapp live location, hapa pia hawezi fanya.

La mwisho, ukiambiwa uko wapi mwambie nipo Namanga, ambapo ni karibia na Kenya ,ukiaambiwa mzigo umefika we waambie ntaufata mwenywe ndani ya huo muda ntakua nishafika.


Kwa kesi ya yule jamaa angu alietaka tapeliwa, niliogelea matusi ya kutosha sana baada ya kumwambia mie nishakujua we tapeli[emoji1][emoji1]
 
Pia ndugu zangu wa Tanzania, kuna hawa matapeli wanaliza sana watu hasa FB na insta wengi wanatumia majina ya watu maarufu na mashuhuri kama Dr. TULIA, PM wa Tz Majaliwa, Nayce Moshi wa Tilisho, Nandy, Chief Godlove, Waganga wa kienyeji.

Hao wote hapo juu ni matapeli na wala hizo sio official accs za wahusika.

Wengi wao wanatangaza ajira za kazi na mikopo ya online.

1. TUKIANZA NA MIKOPO
Hapa utakutana na Tulia Trust mikopo online na majina mengine yenye tulia, utakutana Mo DEWJI foundation, TALA mikopo online and alikes.

Hawa wote wana operate the same, ukiclick link yao ambayo itakua imepostiwa aidha fb au insta itakuleta moja kwa moja whatsapp.

Huko sasa ukituma sms unapata auto reply ya kutuma majina matatu, picha 2 full, mkoa na kazi unayofanya.

Kama utakua mjinga ukatuma hivyo basi utaendelea na hatua nyingine ambayo utapewa kiasi cha riba au installment ambacho unaweka kama kianzio ili kupata mkopo. Mfano ,unataka milioni 1 weka kianzio cha laki 1 etc.

Ukikubali hiyo hatua, wanakupa namba then utafanya muamala. Baada ya hapo utasubiri hadi uchoke hutopata kitu na wata kublock.

Endapo utatuma picha na taarifa zako zingine,LAKINK ukashindwa kulipia aidha kwa kujua kuwa ni matapeli basi watatumia pichazako kukuchafua mitandaoni.

2. WATOA AJIRA
Hapa utakutana na Nandy supermarket, Nayce Moshi etc wao pia watatka taarifa zako kama hapo juu lakini watakutaka ulipie kama laki 1 ili ushonewe nguo za kazi then ukianza kazi utakuwa unakatwa mdogo mdogo. Kama ukawa tahira ukaingia kingi basi utaliwa kichwa na kula block.

3. MAOMBEZI NA KAFARA.
Hapa kuna Masanja mkandamizaji, Mwamposa, Chief Godlove etc. Hao pia huja na lugha za kichurch hurch kama vile karibu mwanangu nikuombee etc, watakutakuta utoe sadaka ili uombewe ukiwa bwege ukatoa itakua umechangia msosi boya mmoja wa pale Manzese ale.

Kwa kesi ya Chief Godlove, yeye anataka utoe admission fee ya 200k ili upate fomu na pete ya bahati. Ukiingia mkenge imekula kwako.

4. VITUO VYA WATOTO YATIMA
Kuna mmoja anajifanya anahusika na watoto yatima kuwaombea msaada mtandaoni. Ila ukitaka mgombane muulize kituo kikowapi uende kupeleka misaada physically au address ya sehemu kilipo HUTOJIBIWA.



NAMNA WANAVYO OPERATE
1. Wanakua na fake accs nyingi za kupost na kukoment wao kwa wao. Wengi wao wanakoment kwa kushukuru kuwa wamepataka kazi, wameponywa.

Chukua muda pitia hio timelines zao, hawana engagements za kutosha kama vile like, comments, posts pia wanakua na marafiki wachache sana.

2. Wanazuia kukomenti na pia ukikomenti kinyume na wao komenti yako inafutwa.

3. Hizo komenti nyingi ambazo ni za kwao lengo huwa ni kuwaaminisha umma kuwa wao ni legit hivyo mtu akiona anafanya hima kufata matakwa yao.


JINSI YA KUWABANA.
1. Ukifanikisha kuwacheki whatsapp ukafata maelezo yao, kabla ya kulipia omba upewe location ya ofisi yao. Hapa wengi watasema wana operate online hivyo hawawezi toa location ya ofisi na kama watatoa wengi watasema wako Nsalaga (Tulia mikopo) , Mo dewji (Dodoma uhindini), Posta ya zamani(Jokate mikopo) sasa wewe waambie wakutumie live location uweze kuwa track UTAKULA TUSI unawekwa block.



Kwa leo niishie hapa
 
Hao ni Matapeli wanakuwaga wapo Mikocheni tu hapo
 
Unapigwa mchana kweupeee, yaani huoni harufu ya utapeli hapo? Hizo mambo washaambiwa watu kibao. Halafu uliona wapi mtu anakuwa tajiri baada ya kumiliki iphone16?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…