Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Kuna mtindo wa kitoto, kijinga, kishamba na ulimbukeni unaokuwa kwa kasi miongoni mwa vijana wa sasa kujivunia kukimbiza magari ovyo ovyo mitaani, yaani kuanzisha ligi na mtu yoyote wanayemkuta barabarani hususani safarini maeneo ya high way, akiwa anaendesha gari yake, basi ghafla hupambana kumpita ili kujivunia ukimbizaji wake na aina ya gari anayoendesha. Nasema hii ni tabia ya kitoto na hatari.
Yaani yuko tayari kununua gari fulani fulani ili aje kufanya hizo ligi zisizo rasmi barabarani halafu aje mitaani na mitandaoni kujigamba na kujitamba.
Yaani kijana kumiliki gari (wengine magari ya wazazi wao, marafiki nk) anataka kila mtu ajue ana gari, anajua kulikimbiza nk.
Sote tunajua barabara zetu zina watumiaji wengi tena ovyo ovyo, ubora na upana kwa sehemu nyingi ni mdogo, magari mengi ni mikweche iliyotumika na kuchoka huko Ulaya, Marekani na Japan kisha ikatupwa hapa nchini, sasa hizo mbio za nini?
Kama wewe unapenda kukimbiza magari nenda rasmi kwenye mashindano ya magari, huko kuna taratibu na kanuni zake, kashindane huko.