As salaam alaykum.
Binafsi zitakuja teknolojia zote lakini hii ya Ndege kupaa kwakweli inanifikirisha sana. Imagine hizi Airbus zinaruka hewani na kutua kama vile hamna kitu kwakweli hapana hata AI ikasome.
Vipi wewe teknolojia ipi inakushangaza?
AI ni more complex kuliko ndege ,ni vile watu hawajui hili, AI mpaka umeweza kuitumia ni maelfu ya data/energy zimetumika/zinatumika kurun the programmed intelligence ya kutambua mambo mbalimbali, hata hiyo ndege yenyewe inaundwa na parts nyingi tu endeshi kutoka ktk mifumo ya AI.
Ugumu wa ndege ni sababu ina high risk kwa maisha ya watu compared na AI ambazo hazina risk zaidi ya gharama za kichumi katika uendeshaji wa mitambo kwenye data center kunakohitaji matumizi makubwa ya nishati ya umeme, matilio ya kupooza mitambo endeshi, human expertisers(data scientist, data engineers), reliable/network infrastructure, upgradable hardware tools kama vile NVDIA GPUs, storage systems n.k,.
Kiufupi ku run project moja tu ya kuendesha AI inahusika mabilioni ya pesa na wataalamu wengi wa sayansi ya kifizikia, biolojia, lugha, mahesabu, saikolojia, uchumi, historia na mambo mengi.
AI iko mbali kwa ubunifu kulinganisha na technology zingine ambazo zimepitwa na wakati, hii bado iko ktk development na hatujui ikiifikia ile peak ambayo wataalamu wanatamani kufikia itakuwaje
Na hii ndio technology ambayo ndio habari ya mjini kwa wasomi wa dunia ya kwanza, huko wanapambana/kushindana kuona ni yupi atashika sehemu kubwa ya mifumo ya AI wakati huo sisi shithole countries bado tunapigana na kurudishana nyuma..