Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kumeibuka kundi la Watanzania ambao wanakerwa sana na Watanzania wenzao wanaomkubali Kagame. Hili kundi lililojivisha kilemba cha uzalendo wanawachukulia Watanzania wenzao wasiomchukia Kagame kama vile ni wasaliti wa nchi. Hii sio sawa, hakuna mwenye hatimiliki ya uzalendo.
Kama wewe unamchukia Kagame kwa kuamini yeye ndiye chanzo cha matatizo yote ya Congo wapo wengine pia wenye mawazo tofauti na hayo.
Wapo wengine wanaofikiri ameifanya Rwanda kuwa nchi nzuri kwa mambo wanayoyapenda wao na kuyapa kipaumbele. Mtanzania kumkubali Kagame isihesabiwe ni usaliti kwa nchi yake au kukosa uzalendo.