Ni uzembe kuendelea kuipamba Dar kwa flyovers wakati shuleni na hospitalini hakuna nyumba na vifaa vya kutosha

Chadema akili zenu zimeenda na mafuriko ya jana. Hivi unataka kusema shughuli zingine zote zisimame, yaani ujenzi wa barabara na vitu vyake visimame zijengwe shule tu na mahospitali?
Jpm kachagua hivyo msivyopenda, vumilieni au jengeni kataifa kenu pale ufipa muwekeze nguvu eneo mnaloona ni sahihi.
Tafuta takwimu kisha angalia ongezeko la shule na hospitali toka jpm anaingia mpaka sasa!
 
Mapato ya Nchi hii asilimia 80 yanatoka Dar es salaam. Unajua hilo?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni mpaka Chato ambako umejengwa uwanja wa ndege wa kimataifa. Wakiwaambia maendeleo ya watu, wao wanaleta propoganda kuwa mbona hamtembei kwa miguu kufanya kampeni, mara mbona Zitto kapanda ndege za Magufuli, mbona amepata huduma ya kwanza katika dispensari ya kijiji! CCM imetengeneza kizazi cha utaahira ambacho itachukua karne kuufuta.
 
Nibahati mbaya tanzania tunamali nyingi lakini shida ipo kwa walioshika uongozi mfano hapa kigoma hatuna vitu vingi tu pamoja na uwanja wampira pia hatuna sasa unapopata kiongozi mbumbumbu atakimbilia kujenga kiwanja cha mpira bilakuangaliakitugani hakipo ambacho wanamichezo nawasiokuwa wanamichezo nimuhim kwamaisha yakila siku
 
Inaonekana hujawai fika Dar au huna ndugu Dar. Tuache na Dar yetu tuendelee kuenjoy.
 
Shida yako wewe huishi kama jina lako la Mchunguzi. Wewe ni mlalamikaji tuu asiyefanya uchunguzi. Ungechunguza ungeona kuwa sababu za kujenga flyovers ni kupunguza foleni jijini Dar es Salaam. Foleni hizi (ambazo siyo kwa magari ya Dar tuu bali ya nchi nzima) zinagharimu pesa nyingi katika uchumi wetu. Ungeelewa pia kuwa Dar inachangia asilimia nyingi katika uchumi wetu hivyo flyovers za Dar ni muhimu saana.
 
Unawezaje kujipa ufahamu usio wako kiasi hiki? Mji gani duniani hauna foleni? Taja mji mmoja tu! Kama flyover ni suluhu stone town, Zbar ingejaa flyover. Mijini kote tutafafuta usafiri wa uhakika na siyo uendeshaji wa raha, hiyo ni plan ya kijinga na waliotuzidi wameshaondoka huko. Walivyoanza na mwendo kasi wangeendelea hivyo kwa miji yote na wengi wangepark magari isipokuwa wale wa aina yako wanaodhani kila mtu anastahili kuendesha kwa raha.
 
Mapato ya Nchi hii asilimia 80 yanatoka Dar es salaam. Unajua hilo?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
That is nonsense! Mawazo kama hayo niliwahi kuyasikia toka kwa wabunge wa Dar. Niliona ni sawa kwa sifa yao ya kujua kusoma na kuandika. Sitegemei mwenye uelewa aje na takwimu mfu kiasi hiki! Hiyo asilimia umeitoa wapi? Inatoka kwenye kitu gani. Income ya nchi hii iko ktk sekta tatu: Utalii, madini na Kilimo. Ktk hayo matatu lipi liko Dar? Ofisi ya malipo ikiwa Dar wewe unasema Dar inaingiza kipato!! Aibu yako boss!
 
Tuanze pole pole tu, una elimu gani, boss? Naogopa nisijibizane na kijana anayesubili kujiunga na chuo. Hospitali ziko wapi? Majengo ni hospitali? Yeye anazitumia au wewe ukiingia na kukuta syringe unaona n! hospitali!
 
Kwa mpangilio huu wa maneno, yabidi tu nikubali matusi. Uliwahi kutunga insha au bado?
 
Kuna nini dar, Boss? Kipindupindu imekwisha siku hizi? Au Corona ilichukuwa chati?
daa kuna bandari ambayo inakulisha hadi wewe, Dar isipo pitika pengine hata hizo nguo hutoweza kuzivaa, mafuta ya magari yanauzwa sheri yanatokea huko Dar, umeona sasa, mizigo yote, inatokea huko, hiyo gari unayopanda inatokea huko.
 
Yupo sawa asilimia 99 ya uchumi wa mikoa yote Tanzania inategemea Dar. Mkuu tafakari vizuri. Mfano tujaribu kuufunga mkoa wa Dar watanzania watakufa njaa.
 
Plannimg ni fani sio kila mtu anajua.

Dar pekee kodi inayokusanywa ni asilimia 16 unalijua hilo? Hizo flyovers zitaokoa nuda unaopotea barabarani na muda huo utatumika kuzalisha hivyo kodi zaidi itakusanywa na kodi hiyo itatumika kufanya hayo unayoyasema.

CCM inaposema itajenga flyovers maana yake huo ni uwekezaji, na uwekezaji wa leo ni kujenga uwezo zaidi wa kutumia kesho.

Katika uchumi sio suala la kusema niitafanya hiki na hiki bali ni suala la kutengeneza mikakati ya kipato zaidi kwa kujenga uwezo zaidi wa uzalishaji ili sasa kipato hicho kitumike kuboresha zaidi huduma zingine

Usipoimarisha Dar maana yake mapato ya nchi yatashuka hivyo utashindea kuboresha maisha ya wananchi kwa sababu utakuwa na resource chache huku idadi ya watu ikiongezeka.
 
Kama flyover sio suluhu basi tuambie suluhu ya fokeni ni nini? Nenda hapo kenya tu kuna flyover kadhaa, mji wa Bangkok flyover za kumwaga na kote huko zimepunguza sana foleni na kuwezesha shughuli za kiuchumi kuongezeka.

Dar unayoidharau, kwa sekta ya huduma na viwanda inachangia sana pato la taifa.
 
Hujui hasara au upotevu wa mabilioni yanayopotea dar kutokana na muda unaopotea barabarani kwa msongamano wa magari. Dar inahusika na asilimia 60 ya mapato ya taifa. Miundombinu bora ya usafiri itaongeza mabilioni kwenye hazina ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…