barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Chadema akili zenu zimeenda na mafuriko ya jana. Hivi unataka kusema shughuli zingine zote zisimame, yaani ujenzi wa barabara na vitu vyake visimame zijengwe shule tu na mahospitali?Nimeona clip ya Polepole akimsifu Magufuli wakati akisoma kitabu ambacho nadhani ni ilani ya chama. Anachokitaja ni idadi ya flyovers zinazopangwa kujengwa; Moroko, Tazara, Magomeni, Mwenge, Chang’ombe na uhasibu, fire, Kinondoni, etc. Huu ni uhuni na ushenzi wa matumizi ya pesa ya taifa hili. Ni uhuni kwa sababu. Pesa ya nchi isigeuzwe kuwa ni pesa ya kuipamba Dar es Salaam kwa sababu za kisiasa. Nchi hii bado sana! Tuna mahitaji kibao.
Kinachosikitisha ni mahitaji mengi tuliyonayo kwenye mambo ya msingi. Shule zetu bado zinaonekana kama mabanda ya wakimbizi. Shule hazina nyumba za waalimu, hakuna maabara, hazina waalimu, hazina vifaa vya sayansi na matokeo yake watoto wote wa shule za vijijini hakuna anayesoma sayansi. Wanasoma masomo wanayoyaita ya arts wakati Kiingereza hawajui kabisa! Hospitali wanazojenga hazina vifaa, nyumba za watumishi hakuna! Sifa za aina hii ni upuuzi mkubwa sana!
Anayewaandikia hizo ilani ana matatizo na hii ndo mbunge mmoja wa CCM aliwahi kuwaita vijana wa Oysterbay! Hawa wanadhani TZ ni Dar tu! Itakuwa bahati mbaya sana kama kweli awamu ijayo itakuwa ni ya kujenga flyover Dar, barabara Dodoma na kuamini ndo maendeleo. Nchi hii ni kubwa.
Jpm kachagua hivyo msivyopenda, vumilieni au jengeni kataifa kenu pale ufipa muwekeze nguvu eneo mnaloona ni sahihi.
Tafuta takwimu kisha angalia ongezeko la shule na hospitali toka jpm anaingia mpaka sasa!