Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kama uhai na utu wa mwanadamu una thamani Tanzania, ni vema hawa watu wanne, Kingai, Jumanne, Goodluck na Mahita, wangekamatwa kwaajili ya kuwafanyia uchunguzi wa kijanai kuhusiana na mazingira yanayowazunguka kuhusu kuwatesa watu, kuwateka, kuwapoteza na hata mauaji.
Majina haya manne yanatajwa tajwa sana kuhusiana na matukio ya utekaji, upotezwaji na hata mauaji ya watu mbalimbali.
Katika hali ya kawaida, tungebahatika kuwa na utawala/uongozi unaojali haki za msingi za raia na sheria za nchi, hawa walistahili kukamatwa na kuhojiwa juu ya uhusika wao katika utekaji, upotezwaji na mauaji ya watu. Kama walihusika wafikishwe mahakamani, kama hawakuhusika, basi wapate kutakaswa.
Wahanga mbalimbali wa matukio ya utekaji, wameweza kuwatambua hawa watu kama miongoni mwa watesi wao. Kwa nini wasikamatwe na kuchunguzwa?