Ni Vema Kingai, Jumanne, Goodluck na Mahita Wangekamatwa

Ni Vema Kingai, Jumanne, Goodluck na Mahita Wangekamatwa

Kushitakiwa hawa watu ni ngumu sababu ni ngumu kutenganisha polisi na mhimili uliojichimbia sana (CCM) tofauti yao ni ndogo sana.
 
Yawezekana mbinu za interrogation ndio shida,labda mafunzo yao yana walakini.Labda kwa kutojua wanajikuta wanatumia nguvu nyingi kupindukia wakidhani ndio watapata confession ya mtuhumiwa.
Mbona hata NAZI Germany ilimuandika kazi chief interrogator Hanns Scharff yeye alikuwa hatumii nguvu,yupo tiyari atoke na mfungwa ampe uhuru hata atamununulia chakula au kinywaji hadi mtuhumiwa mwenyewe anakiri makosa yake bila nguvu.Na hiyo ni vita ya pili.Iweje leo bado watesaji hawajifunzi?

Hanns Scharff-L.png
 
Kama uhai na utu wa mwanadamu una thamani Tanzania, ni vema hawa watu wanne, Kingai, Jumanne, Goodluck na Mahita, wangekamatwa kwaajili ya kuwafanyia uchunguzi wa kijanai kuhusiana na mazingira yanayowazunguka kuhusu kuwatesa watu, kuwateka, kuwapoteza na hata mauaji.

Majina haya manne yanatajwa tajwa sana kuhusiana na matukio ya utekaji, upotezwaji na hata mauaji ya watu mbalimbali.

Katika hali ya kawaida, tungebahatika kuwa na utawala/uongozi unaojali haki za msingi za raia na sheria za nchi, hawa walistahili kukamatwa na kuhojiwa juu ya uhusika wao katika utekaji, upotezwaji na mauaji ya watu. Kama walihusika wafikishwe mahakamani, kama hawakuhusika, basi wapate kutakaswa.

Wahanga mbalimbali wa matukio ya utekaji, wameweza kuwatambua hawa watu kama miongoni mwa watesi wao. Kwa nini wasikamatwe na kuchunguzwa?
Kwani Tz hakuna tume ya haki za binadamu au taasisi yeyote ya kutetea haki za kuishi kwa mwanadamu.Bahati mbaya sana sikusoma sheria,ningewafikisha kwenye mahakama za kimataifa za hapa tz Ni za ccm .
 
Damu na roho za marehemu wote na ziwe juu yao na vizazi vyao.Ameen...!
 
Back
Top Bottom