Huenda Simba SC ikawakosa wachezaji tegemeo, Sadio Kanoute (Box to Box Midfielder) na Joash Onyango (Defender) kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC, kati ya Simba SC dhidi ya Orlando Pirates April 17, 2022 kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.
Baadhi ya Mashabiki wa Simba na Wadau wa Kabumbu Nchini Tanzania wamekuwa na maoni tofauti kwenye kupanga Kikosi cha Simba SC.
Asilimia kubwa wanaamini Taddeo Lwanga kuanza badala ya Mzamiru Yassin na Kennedy kuanza badala ya Wawa.
Utabiri Wangu: Manula, Kapombe, Hussein, Ennock, Kennedy, Mkude, Mzamiru, Sakho, Bwalya, Mugalu, Morrison.
Je kwa upande wako una lipi katika hili..?!