Ni vigezo gani vimetumika kustaafisha jezi namba 20 Simba?

Ni vigezo gani vimetumika kustaafisha jezi namba 20 Simba?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
0A69DAD8-7954-446D-8421-CF1F8636C757.jpeg
 
Ko tuseme wanamhadaa tu???
Au tuseme hajui mpira, au tusema hamna shukurani??.
 
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Naongezea"Liver hawajastaafisha jezi ya GERRARD "
 
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Mkuu hebu kwanza Relax maana hayo ni maamuzi Tu, kwa sababu ata wakwambie hicho kitu Cha maana alichokifanya Mkude inawezekana kwako usione kama ni cha maana

Neno "Maana" lina tafsiri nyingi inategemea litatumika wapi na kwa yupi, mwingine kumiliki Gari kwake ni Jambo la maana ila mwingine haoni umaana wake, na haifanyi lisiwe na maana eti kwa sababu yeye kaona halina Maana

Pale kwa watani wetu Yanga, saizi kila wanapoenda wanatembea na Medali zao za second runner wa kombe la shirikisho, ilhali hilo kombe lina Bingwa tu huyo mwingine hostoria yake inaishia hapo

Tumeozea kuona habari za Mshindi wa pili kwenye Riadha na mashindano yote ya Olympics, Lakini wao wameona hilo ni la Maana na wanasherekea ila huwezi kuona Inter Milan/Roma inasherekea ushindi wa pili wa UEFA/EUROPA

Kwahiyo hadi hapo tunakubaliana kuwa Neno maana ni maamuzi tu ya watumiaji,Anyway kwa ufupi tu kutoka kwangu shabiki na sio kiongozi, sababu ambazo naona kwangu zina Mashiko

Mkude ndio mchezaji Pekee katika ligi ya NBC alietokea katika kikosi cha vijana na kwenda senior timu na kudumu kwa miaka 13

Mkude ndio mchezaji Pekee ambae ameshinda mataji mengi kuliko mchezaji mchezaji mwingine yoyote pale Simba katika Zama zake

Mkude ndio mchezaji pekee ambae amedumu katika nyakati zote pale Simba, Yani nyakati za Njaa na ahueni, alikuwa anaweza kuondoka kama wachezaji wengine ila aliamua kubaki

Mkude ndio mchezaji Pekee ambae amekuwa akipitia vipindi vigumu katika nyakati tofauti tofauti na club kutokana na utovu wake wa nidhamu ila kwa pamoja waliendelea kuvumiliana

Mkude ni kama Nembo ya club ya Simba, ni kama vile Gerrard pale Liverpool,Lampard pale Chelsea,Tony Adams pale Arsenal,Raul pale Real Madrid,Paul scholes Man utd nk

Mkude ni Alama ya Mchezaji kuwa loyal, na anaoesha kuwa ata vijana wengine wanaweza kutokea team za vijana na hatimae kucheza kwa mafanikio na hatimae kudumu kwa muda mrefu katika senior team

Kuhusu kwanini hao wengine katika team zao kama Gerrard or Lampard jersey zao hazijastaafishwa sie hayatuhusu maana ni maamuzi ya Club husika na huwezi kuwapangia

Kwahiyo mkuu we kaa na hivyo vyako unanoviona vya maana, ila Kwa Simba kwao Mkude kafanya vingi vya maana sana kuweza kumpa hiyo Heshima ambayo wao wameona inafaa apewe

Mnaacha kushangaa huko makwenu mmestaafisha hadi sahani/vikombe/glass/hotpot/kiti kuwa hivi vitu ni vya Baba mwenye nyumba hatumii mtu mwingine yoyote uje kushangaa Mkude kustaafishiwa jersey yake
 
Hao kina barca na juve ni maamuzi yao na simba ni maamuzi yao.
 
Ujue Timu zetu zinaendeshwa na mihemko.

Mkude hakuna la Maana amewahi fanya Simba.

Maana yake watastaafisha na 22 ya Bocco
 
Ujue Timu zetu zinaendeshwa na mihemko.

Mkude hakuna la Maana amewahi fanya Simba.

Maana yake watastaafisha na 22 ya Bocco
Kwanza tukubaliane kwamba maamuzi ya kustaafisha jezi ya Jonas Mkude hayakupangwa toka awali bali yamekuja baada ya ile "THANK YOU" yake ambayo haikuwa tofauti na ya Nelson Okwa na nyie watu wa mitandao mkaanza kuwazodoa Simba kwamba hawawajeshimu Malejendari wa timu. Kwa hiyo ukatengenezwa mkakati wa haraka haraka nini kifanyike kupoza maneno hayo ndo likazaliwa wazo la kustaafisha jezi yake ambalo sioni ubaya wake na pia ikaahidiwa aagwe rasmi siku ya Simba day kama alivyofanyiwa Medie Kagere msimu uliopita. Swali linabaki, Je katika msimu huu wa usajili Jonas Gerard Mkude akiamua kusaini Yanga hata Kwa mkataba wa miezi sita ataalikwa kuagwa kwa heshima Simba day? Timu za Kariakoo zinajulikana Kwa fitina, watakaokuwa waajiri wapya àmbao wanaweza kumuajiri ili tu kuonyesha wenzao kwamba wamemuonea kama ilivyowahi kufanyika huko nyuma Kwa baadhi ya Wachezaji na makocha watakubali aende siku hiyo? (Anyway Hilo niliache Kwa vile halijatokea).
Nibaki na hili la jezi No.20 kupewa heshima ya kipekee ya kutoonekana kwenye timu ya Simba mpaka atakapotikea mchezaji mwenye Kariba ya Jonas Gerard Mkude. Binafsi naona vigezo walivyotumia vinatosha maana havijawahi kufikiwa na mchezaji mwingine zaidi ya Mkude. Hakuna mchezaji ndani ya Simba aliyewahi kuanzia timu ya vijana (siyo academy) hadi senior team akacheza Kwa mafanikio kikosi cha Kwanza kiasi cha kuwa kiungo tegemeo Kwa miaka 13 mfululizo bila kuhama zaidi ya kufungiwa na timu yenyewe Kwa vipindi fulani kutokana na kushuka Kwa nidhamu yake kitu ambacho huwezi kukikwepa maana kinamkumba Mtumishi yeyote kwenye Taasisi. Pale Man Utd Mtoto mpeñdwa wa Old Trafford tangu akiwa kinda David Beckham aliwahi kutupiwa kiatu na kujeruhiwa jicho na kocha gwiji na Kipenzi cha Waingereza wote Sir Alex Ferguson na ikapelekea kuuzwa. Hata vikombe ndani ya kabati kuna kipindi vinagingana bila kusukumwa kisa tu vilikaa vibaya baada ya mmiliki kutoa sahani.
Nenda Kwa Amani Jonas Gerard Mkude, tembea kifua mbele maana unamalizia kizazi cha Wachezaji Wenye vipaji binafsi ambavyo havikutokana na shule. Ni kama Wayne Rooney alivyohitimisha kizazi cha vipaji asilia cha washambuliaji pale England na Sasa tunashuhudia broilers wasioweza kubadilisha chochote mpaka Kwa maelekezo ya Mwalimu.
Kwangu heshima uliyopewa inakustahili, tena nakuombea upate timu ya kiwango cha Kati juu ambayo itakubakiza kwenye ramani usije ukapotea kama rafiki yako Yondani na Juma Nyosso.
 
Simba tuliwahi kustaafisha jezi namba 30 ya marehemu Petii Mutesa Mafisango lakini alipokuja Kakolanya akaivaa🤣🤣
 
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Kwa hiyo umeumia sana siyo? Kunya boga basi
 
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Zipo namba nyingi tu mkuu za kuvaa, hiyo 20 kitu gani bhana ?
 
Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?

Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?

Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.

Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Kwani unateseka nn hebu tufanye jezi imestaafishwa maana hakuwa na mchango wowote simba over. Ukianza kuleta maana kwenye maamuzi ya watu utakua zezeta
 
Back
Top Bottom