Mkude amefanya nini la maana Simba Sports mpaka jezi namba 20 aliyokuwa anavaa kustaafishwa?
Sijaona Barcelona wakistaafisha jezi ya Messi, Man Utd wakistaafisha jezi ya Giggs au Ronaldo?
Ac Milan wamestaafisha jezi namba 3 ya Maldini kwakuwa alifanya makubwa sana ndani ya Milan akiwa kama Captain na hakuwahi kuhama.
Sasa mkude ambaye alivuliwa hadi unahodha kwa utukutu ana nini cha uspecial?
View attachment 2670674
Mkuu hebu kwanza Relax maana hayo ni maamuzi Tu, kwa sababu ata wakwambie hicho kitu Cha maana alichokifanya Mkude inawezekana kwako usione kama ni cha maana
Neno "Maana" lina tafsiri nyingi inategemea litatumika wapi na kwa yupi, mwingine kumiliki Gari kwake ni Jambo la maana ila mwingine haoni umaana wake, na haifanyi lisiwe na maana eti kwa sababu yeye kaona halina Maana
Pale kwa watani wetu Yanga, saizi kila wanapoenda wanatembea na Medali zao za second runner wa kombe la shirikisho, ilhali hilo kombe lina Bingwa tu huyo mwingine hostoria yake inaishia hapo
Tumeozea kuona habari za Mshindi wa pili kwenye Riadha na mashindano yote ya Olympics, Lakini wao wameona hilo ni la Maana na wanasherekea ila huwezi kuona Inter Milan/Roma inasherekea ushindi wa pili wa UEFA/EUROPA
Kwahiyo hadi hapo tunakubaliana kuwa Neno maana ni maamuzi tu ya watumiaji,Anyway kwa ufupi tu kutoka kwangu shabiki na sio kiongozi, sababu ambazo naona kwangu zina Mashiko
Mkude ndio mchezaji Pekee katika ligi ya NBC alietokea katika kikosi cha vijana na kwenda senior timu na kudumu kwa miaka 13
Mkude ndio mchezaji Pekee ambae ameshinda mataji mengi kuliko mchezaji mchezaji mwingine yoyote pale Simba katika Zama zake
Mkude ndio mchezaji pekee ambae amedumu katika nyakati zote pale Simba, Yani nyakati za Njaa na ahueni, alikuwa anaweza kuondoka kama wachezaji wengine ila aliamua kubaki
Mkude ndio mchezaji Pekee ambae amekuwa akipitia vipindi vigumu katika nyakati tofauti tofauti na club kutokana na utovu wake wa nidhamu ila kwa pamoja waliendelea kuvumiliana
Mkude ni kama Nembo ya club ya Simba, ni kama vile Gerrard pale Liverpool,Lampard pale Chelsea,Tony Adams pale Arsenal,Raul pale Real Madrid,Paul scholes Man utd nk
Mkude ni Alama ya Mchezaji kuwa loyal, na anaoesha kuwa ata vijana wengine wanaweza kutokea team za vijana na hatimae kucheza kwa mafanikio na hatimae kudumu kwa muda mrefu katika senior team
Kuhusu kwanini hao wengine katika team zao kama Gerrard or Lampard jersey zao hazijastaafishwa sie hayatuhusu maana ni maamuzi ya Club husika na huwezi kuwapangia
Kwahiyo mkuu we kaa na hivyo vyako unanoviona vya maana, ila Kwa Simba kwao Mkude kafanya vingi vya maana sana kuweza kumpa hiyo Heshima ambayo wao wameona inafaa apewe
Mnaacha kushangaa huko makwenu mmestaafisha hadi sahani/vikombe/glass/hotpot/kiti kuwa hivi vitu ni vya Baba mwenye nyumba hatumii mtu mwingine yoyote uje kushangaa Mkude kustaafishiwa jersey yake