Maigizo, hio mipango ipo sana tangu enzi za Mwinyi
Mkuu nakubaliana nawe mipango ipo miaka mingi.
Nimesoma kitabu cha Mwinyi "Mzee Rukhsa : Safari ya Maisha Yangu".
Ukurasa wa 136 anaelezea alivyotembelea Korea ya Kaskazini tarehe 7 mpaka 23 April 1985, akiwa Makamu wa Rais. Akasaini mikataba ya kilimo cha umwagiliaji na shamba la pamoja la hekta 100,000 katuka bonde la mto Rufiji. Wakipanga kila hekta hata ikizalisha tani 10 za mahindi na mpunga, kuwe na tani 2,000,000 za chakula kwa mwaka.
Lakini Mwinyi anasema shamba halikuwahi kulimwa lote wala kufikia tija hiyo.
Pia kulikuwa na mpango mwingine wa kulima pamba hekta 100,000 kanda ya ziwa. Habari ni ile ile, mpango haukufanikiwa.
Kwa hiyo una kila sababu ya kusema mipango hii ilikuwapo tangu enzi za Mwinyi, Mwinyi mwenyewe kaandika.
Ila huoni kwamba watu kama kina Bashe wanaleta matumaini mapya?
Mimi naona tatizo la kimfumo ni kubwa sana na inawezekana watu wachache tu hata wakiwa na ideas nzuri vipi wakashindwa.
Sasa wewe umefanya nini kujiongeza tuondoke hapa tupige hatua zinazotakiwa?
Sasa hapa kwenye matatizo ya kimfumo tunafanya vipi?
Maana ni rahisi kulaumu wengine, wewe umefanya nini?