Heri ya Mwaka mpya wa 2012!!
Ukiwa ni mwanzo wa mwaka 2012 napenda kushirikiana na wana jamvi juu ya jambo mojawapo nililokuwa nalifikiria sana katika mwaka uliopita; nalo ni Rais wa Tanzania (ama Tanganyika) wa awamu ya tano(5) awe na sifa gani?
Naamini kama nchi mafanikio hayaji kwa kubahatisha au kwamba wengine walaaniwe na sisi tubakie tuliobarikiwa; bali huja kwa kukusudia.
Some people succeed because they are destined to, but most people succeed because they are determined to. ˜-Author unknown.
Kutokana na pale tulipo kama nchi, mtu mwenye akili akija kututathmini atatuonea huruma sana. Na mwingine anaweza kusema Peter Botha alisema ukweli juu watu weusi japo kauli yake ilikuwa ya kibaguzi zaidi
. By now every one of us has seen it practically that the Blacks cannot rule themselves. Give them guns and they will kill each other. They are good in nothing else but making noise, dancing, marrying many wives and indulging in sex. Let us all accept that the Black man is the symbol of poverty, mental inferiority, laziness and emotional incompetence
And here is a creature that lacks foresight. There is a need for us to combat him in long term projections that he cannot suspect. The average Black does not plan his life beyond a year. Peter Botha
Lakini ukweli unabakia kuwa sisi tunaweza, tatizo wenye kutuongoza si viongozi na wenye kututawala si watawala. Hawakujijali kauli hii
As long as I am a leader, our position is not going from that of our forefathers. I do not want the responsibility for selling the rights of our children yet unborn. – unknown author.
Kufikiri kwangu kulinipeleka kuona sifa hizi zifuatazo:
Asiwe na uhusiano na mtandao wowote wa kifisadi
Ili aweze kuiongoza Tanzania huru bila ya shinikizo la watu wengine wanaomongoza kwa remote hasa mafisadi, ni LAZIMA asiwe na ushirika wowote na mtandao huo. Vinginevyo hatufai, atakuwa janga.
Asitoke CCM
Najua wako wengi watanishambulia katika point hii, lakini ndiyo ukweli. Rais ajaye hafai kutoka CCM, akiwa mwana CCM ni kujiongezea janga jingine. CCM yenye kuwajali wakulima na wafanyakazi imekwisha potea. Haiwezekani kumpata kiongozi miongoni mwa hawa waliopo katika CCM atakaye kuwa na uchungu na wakulima na wafanyakazi na kufikiri ustawi wao wakati huohuo akawasahau CCM wenzake ambao walio "wabinafsi/walafi". Ikiwa unafikiri yupo mwenye uchungu katika hili ama kwa kauli na vitendo mtaje. Wengi watasema tu, kwenye vitendo mgogoro. Ndiyo
Awe na isfa na ujasiri wa kuuvunja mtandao wa kifisadi
Ili Tanzania itoke katika hali ngumu ya maisha iliyonayo sasa na kufufuka kiuchumi ni
LAZIMA Rais ajaye awe na ubavu wa kuubomoa mtandao wa mafisadi. Hawa wanaotajwatajwa CCM kwamba wanawania urais 2015 hawawezi kusema kwamba wana ubavu wa kuuvunja mtandao huo ikiwa wa nao wamenufaika na mtandao wenyewe. Ni lazima kwa Rais ,si kuubomoa tu mtandao huo bali pia, kuwashitaki wahusika wote katika mashitaka yayatayoipatia ushindi Serikali (Umma wa watanzania) dhidi ya mafisadi hao.
Mwenye maono ya kuijenga Ikulu na kutunza heshima yake
Heshima ya Ikulu imeporomoka mno mno. Sasa kinaonekana kama kijiwe cha "wahuni" Fulani wakati ni taasisi yenye heshima ya juu Tanzania. Kuna minong'ono kuwa mfumo wa utendaji kazi wa Ikulu(kwa maana ya watendaji wake) umeparaganyika. Walioingia baadaye wakafikiri wanajua kuliko waliokuwepo awali nao wamechangia kuivuruga nidhamu na uwajibika wa Taasisi hii. Kwasasa huwezi kumwambia mtu mwenye "akili" ,Ikulu ni mahalali patakatifu akakubaliana nawe, kama si kukudharau.
Anayeweza kuvitumia vichwa vya wataalamu mbalimbali kuijenga Tanzania
Rais hajui kila kitu kuhusu Tanzania; hajui kila kitu kuhusu fani zote kuanzia kwenye kilimo hadi kwenye viwaanda; michezo hadi utamaduni; elimu hadi uchumi. Anahitaji kuwa ni mtu msikivu na anayeshaurika, na anayeweza kutumia vichwa mbalimbali vya wataalamu katika kuijenga Tanzania.
Anayeweza kusoma na kuzithamini tafiti mbalimbali na kuziiingiza katika sera kama si kuboresha utendaji wa serikali
Rais anayekuja ni
LAZIMA awe anasoma, kama si yeye mwenyewe moja kwa moja basi kupitia wasaidizi wake tafiti mbalimbali za wanataaluma wa ndani. Kisha kuzitumia kwa ustawi wa jamii ya watanzania kwa kuziingiza katika sera. Pia zaweza kutumika kuboresha utendaji wa serikali ama taasisi za serikali.
Ni bahati mbaya kubwa sana ya kwamba ziko tafiti nyingi zimefanywa lakini matokeo yake ni kuwekwa katika maktaba za vyuo au taasisi husika. Nchi za wenzetu wanatumia kazi za utafiti kustawisha jamii zao, lakini kwetu…ni jambo lahuzini.
Anayethamini utu wa mtu
Hatuhitaji Rais anayethamini mali ya mtu au kile alichonacho mtu bali, kwanza athamini utu wa mtu kisha mchango wa mtu katika kuijenga jamii huru yenye matumaini ya ustawi wake bila ya kudhalilishwa.