Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,933
- 988
Hizo sifa ni muhimu sana..maana huyo rais atakuwa na kaz kubwa..yakuirudisha tanzania kwenye nafasi ya kuwa nchi yenye kuthamin mali zetu....nakusihi Mungu utusikie maombi yetu.
Amina!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hizo sifa ni muhimu sana..maana huyo rais atakuwa na kaz kubwa..yakuirudisha tanzania kwenye nafasi ya kuwa nchi yenye kuthamin mali zetu....nakusihi Mungu utusikie maombi yetu.
Ndugu wa JF,
Wote tunafahamu baadhi ya majina ya wanasiasa ambao wamekua wakitajwa kuwania nafasi ya Urais mwaka 2015. Bila kujali Rais atatoka chama gani, ni vyema watanzania tuelewe tunahitaji mtu mwenye sifa gani hata kabla ya uchaguzi. Kwa mtazamo wangu, Rais ajae awe angalau na sifa hizi:
1. Mwenye ujasiri wa kuilinda Katiba na Sheria za nchi bila woga.
2. Mwenye uwezo na ujasiri wa kuifuta au kuichambua kwa upya mikataba yote isiyo na maslahi kwa Taifa.
3. Ambae hatageuza Ikulu kuwa pango la wanyang'anyi: Yani awe ni mtu anayeichukia rushwa na ambae hataingia Ikulu kwa kutumia rushwa.
4. Ambae hatakuwa na hofu wala aibu ya kumchukulia hatua za kisheria yeyote atakaevunja sheria za nchi bila kujali cheo chake, urafiki, au maslahi binafsi.
5. Mwenye mipango madhubuti na inayotekelezeka ya kuweza kututoa Watanzania katika hatua tulionayo na kufikia hatua nyingine.
6. Ambae atadumisha umoja, undugu, na mshikamano wa Taifa na kukemea kwa nguvu zote chokochoko za udini, ukabila, ukanda, au ushabiki wa kisiasa unaotishia umoja wetu.
Haya ni baadhi tu ya mambo tunayoyataka kwa Rais ajaye. Kwa wale wanaotajwa tajwa sijui nani ana vigezo hivi? Mwisho wa siku ni kura yako ndio itakayoamua nani awe Rais.
Asanteni.
Wanajamvi, Rais J.
Kikwete Amekaribia Kumariza Muda Wake. Anaondoka Madarakani Kukiwa Na
Changamoto Zifuatazo, Mosi, Sintofahamu Mahusiano Mabaya Ya Rwanda Na
Tanzania, Pili, Mgogoro Wa Ziwa Nyasa Kati Ya Malawi Na Tanzania, Tatu,
Kuongezeka Kwa Vitendo Vya Kigaidi,mf.Kulipuliwa Kwa Kanisa La Olast
Arusha,mauaji Ya Padri Mushi, Uchomaji Wa Bar. N.K, Tano, Mchakato Wa
Katiba Mpya Sita, Elimu Ambako Walimu Mishahara Ni Midogo, Shule Za Kata
Hazina Waalimu Wa Kutosha, N.K. Sasa Kutokana Na Changamoto Hizo,
Unadhani Ni Nani Ambae Au Unafikiri Ndiye Mtu Pekee Wa Kumkabidhi
Usukani Wa Kuendesha Gari Letu? Anasifa Zipi Ambazo Unatushawishi Tumpe
Dhamana Hii Kubwa? Pia Amefanya Yepi Mazuri Hadi Tumwamini? Hebu Leteni
Hoja Na Vioja.