Salaam wanajamvi!
Tukielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwakani(2015), majina kadhaa yamekuwa yakitajwa kujaza nafasi itakayoachwa wazi na Rais Dr Kikwete.Nikiwatazama,waheshimiwa hawa, Sita, Membe, Lowasa, Wasira,
Nchimbi,Januari, Kigwangara,Pinda,Mwandosya, Sumaye, Migiro, Tiba n.k ukiwaacha wale wa upinzani, Wamekuwa sio kivutio kwa watu wengi wasioridhishwa na kasi ya maendeleo ya nchi, nidhamu ya viongozi, uwezo wa kiutendaji wa watumishi wakuu wa Umma na uvunaji wenye tija wa rasilimali za nchi.
Ukiacha vikundi vidogo vidogo vinavyowaunga mkono, watu walio wengi wanaona bado hakuna mwenye Haiba na Uwezo kwa nafasi hiyo.Watu wanalazimika kusema nafuu flani kuliko flani, hii inaonesha hakuna wanayeridhika naye bali wanalazimika kufanya chaguo pengine kwa kutokuona kama kuna Watanzania wengine wenye Haiba na uwezo kwa nafasi hiyo. Sina haja ya kufafanua udhaifu wa kila moja ila kwa ujumla sioni kiongozi hata mmoja mwenye kujiamini, mtendaji mzuri,mbunifu,mwenye maono, mwenye akili za kutosha(sina maana ya Elimu), mwenye uhodari wa kuongea anayeweza kujenga hoja akaeleweka na kuiletea heshima nchi yetu.
Ebu tusaidiane wanajamvi wenzangu kuibua na kufahamishana vichwa vya maaana(watu competent), walio ndani na nje wanaoweza kutusaidia, tuwashawishi wajitokeze kwa chama chotechote na tuwaunge mkono, tuachane na hao jamaa juu, ni wepesi muno bajamani.Sio lazima mtu awe amepata kuwa waziri au mbunge ndo kiwe kigezo cha kuwa rais!