Watanzania tumejisahau kwamba kwenye uraisi tunahitaji nini hasa. Kwa mawazo yangu tunahitaji maendeleo nchi yetu ni masikini bado kiuchumi na tunahitaji kiongozi anayeelewa mambo na kutuletea maendeleo. Sasa watu wakianza kuongelea viongozi ambao wanaweza kuwa uraisi wanasema vitu ambavyo ni vya kishabiki zaidi mfano mtu mwenye kula rushwa na kila mtu anajua kuna wanaosema hao wanapedwa kama vile uraisi ni mapenzi pekee au viongozi wengine hawapendwi kibinafsi lakini si kiamaendeleo au kiuwezo. Mimi ninaona tutafute kiongozi atakayetufaa tuachane na mafisadi na mambo ya mapenzi je tukipenda watu ambao wanatuibia au wanakashfa za rushwa watatusaidia nini kwenye nchi yetu? msijamka lalamika kwanini hatuna maendeleo wakati mnachagua wala rushwa mnaowapenda