Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Mshahara ulopendkezwa na TUCTA ni 1, 010,000 kwa mwezi na huo watosha kukabiliana na gharama za maisha.
Kuna masuala kama mfumuko wa bei kwa bidhaa muhimu na pia gharama zingine za maisha kama malipo ya pango, matibabu hospitalini na malipo ya huduma zingine kama umeme na maji.
Lakini serikali ya raisi Samia bado ina kazi ya kubuni mipango sahihi ya kuboresha maisha ya watanzania. Njia mojawapo ni kuhakikisha nchi ina umeme wa uhakika.
Ukiwepo umeme wa uhakika hiyo itasaidia kuwepo kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi kama viwanda, karakana ambavyo vitaweza kulipa gharama nafuu za umeme ambao utazalishwa wa kutosha.
Serikali pia kupitia wizara ya Kilimo ifanye maamuzi ya kwamba sasa kulima kwa jembe kumepitwa na wakati na ianze kwa hatua kuwasaidia wakulima kuagiza vifaa vya kilimo nje ya nchi ili waanze kulima kwa kiwango kikubwa. Pia wakulima hao wasaidiwe kupata mbolea na pembejeo zingine bila urasimu.
Nimefurahishwa na kuona watu kama Masanja sasa aweza kuuza mchele wake unolimwa huko Sangu kwa kupakiwa uzuri katika magunia kwa ujazo tofautifotauti.
Pia wapo wakulima wengine kama bwana Samli kule Sumbawanga lakini bado hiyo haitoshi kwani nchi hii asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji.
Lakini kilimo chahitaji mapinduzi kwa kulima mazao yote kwa kiwango cha juu ili kuweza kuwa na chakula cha kutosha na pia kuweza kuuza hata huko nje ya nchi.
Yawezekana kabisa kwamba hadi mida hii wapo wafanyabiashara ambao wanasafirisha mazao nje ilhali chakula cha kutosha kwa nchi kinakosekana na kusababisha bei kupanda kutokana na kuwepo kwa mahitaji ya juu.
Ufugaji pia wahitaji mapinduzi kwenye namna bora za ufugaji kama vile uwekaji sahihi wa namba za masikioni kidijitali kwa wanyama, utunzaji kumbukumbu, machinjio bora ya utayarishaji bidhaa za zitokanazo na wanyama na mauzo kwenye maduka bora yaani si kila mtu tu auza nyama hata zile zilotokana na wizi wa mifugo.
Tusisahau kwamba mfumuko wa bei (Inflation) huenda na hitaji na kama hitaji hilo au (Demand) ni kubwa na kuna uhaba (scarcity) basi mfumuko wa bei hupanda kwa kasi ya ajabu. Je serikali imefanya utafiti kubaini mfumuko wa bei waanzia wapi? je, uhaba upo wapi? na je wapi panasumbua kwenye uzalishaji na usambazaji wa bidhaa?
Pia je, madukani na kwenye vituo vya mafuta bei zaangaliwa zisizidi viwango? Yajulikana vita ya Russia na Ukraine imepelekea kuwepo na shida ya upatikanaji wa mafuta na gesi duniani je kama nchi tumejiandaa vipi na dharura kama hizi?
Sekta za Kilimo na ufugaji zikiangaliwa uzuri zaweza kabisa kuongeza ajira na hatimae kupunguza idadi ya watu mijini kwa kuamua kurudi mashambani ambapo nako kukiboreshwa uzuri kwa kujengwa miundombinu kama mashule, masoko, mahospitali na shughuli za mabenki na posta hiyo itakuwa njia mojawapo ya nchi kuanza kujikwamua kiuchumi.
Sekta binafsi hukua kutokana na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kiuendeshaji kama vile teknolojia na miundombinu ya kisasa kama barabara khasa za vitongojini. Nchi nyingi ziloendelea zimeachia shughuli za sekta binafsi kufanywa na manispaa husika.
Sekta binafsi haiwezi kulipa mishara minono iwapo hakuna uzalishaji wa kutosha na mapato mazuri kwa biashara kwani sekta hii huendeshwa zaidi na matarajio ya kupata faida kwa haraka.
Baadhi ya shughuli ambazo sekta binafsi yaweza kufunguliwa ikafanya kukiwepo na uhakika wa njia za kiteknolojia na gharama nafuu ni pamoja na uchumi wa kidijitali kama ule uitwao "gig economy" ambao huzihusisha shughuli kama Uber ambazo huweza kuajiri vijana kwa mikataba mifupi na mirefu.
Lakini serikali imeshindwa kuelewana na wenye makampuni haya kama ya Uber khasa kwenye masuala ya urasimu ambapo makampuni haya yahitaji uhuru wa kufanya shughuli zao na pia kulipa mapato ambayo yanatokana na shughuli wanozifanya badala ya kukadiriwa kodi.
Hivyo kusema serikali imekosa watu ambao waweza kuzingalia shughuli hizi za "Gig economy" ambazo zaweza kuiinua sekta binafsi. Mathalani Uber yaweza kufanya shughuli zake kama uchukuzi Taxis) na kusambaza vyakula (food delivery) hivyo kusaidia kutengeneza ajira na pia kupata mapato yatokanayo na kodi.
Ukiangalia sana waona kwamba sekta binafsi ikiangaliwa uzuri yaweza kabisa kuwa yalipa mishahara minono kwa watumishi wake kuzidi wale wa serikali kwasababu sekta hiyo itakuwa ikivutia vijana wamalizao masomo wenye kuleta vipaji murua na kuleta mabadiliko ya uendeshaji wa sekta hiyo kwenye viwanda, makampuni na sehemu zingine za biashara.
Kinotokea sasa hivi katika sekta ya umma ni ubinyaji yaani kwa kiingereza "squeeze" au kubana matumizi lakini huku wanoumia wakiwa ni wafanyakazi haohao. Watumishi wa umma kama walimu, polisi, mahakimu na wengine wote wastahiki kuangaliwa mishahara yao jambo litosaidia kupunguza vitendo vya rushwa, ubadhilifu na kutotoa hukumu sahihi kwa sababu ya kupokea milungula.
Hivyo Kwanza, napendekeza serikali iketi chini na sekta binafsi na kujadili namna bora ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara ili kuongeza tija itayosaidia kuongeza kipato kwa watumishi wa sekta hiyo.
Pili, Serikali ikazanie kukusanya kodi khasa kutoka kwenye biashara kubwa kulingana na mapato ya biashara hizo.
Kodi ndo msingi wa maendeleo katika taifa lolote lile bila kodi hakuna maendeleo na mwisho tunaona yanotokea kama kule Sri-Lanka ambapo nchi yaendeshwa kifalme hadi kusahau kwamba kuna wananchi.
Kila mwananchi alipe kodi ili kuiwezesha serikali kupanga matumizi yake sahihi, na kupunguza madeni au kukopa huko ng'ambo. Serikali ina vyanzo vingi sana vya mapato hivyo haina sababu kabisa ya kusingizia matatizo yanotokea sehemu zingine.
Selikali ikusanye kodi kiufasaha, wananchi walipe kodi stahiki na serikali ipange viwango vya mishahara kulingana na ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mwisho, nchi hii ina utajiri wa kutisha na tumeukalia yaani uchumi tunao ila twaukalia ati. Wananchi wajitahidi kujiinua ili uchumi ukue kwa kuongeza shughuli za uzalishaji na kuchapa kazi.
Mungu ibariki Tanzania.