Ni vikwazo vipi vinadumaza matumizi ya gesi ya kupikia?

Ni vikwazo vipi vinadumaza matumizi ya gesi ya kupikia?

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Wizara ya Nishati imetangaza kuandaa kongamano la nishati safi ya kupikia yaani ‘Clean Cooking Conference’ ili kuchunguza vikwazo vinavyodumaza matumizi ya nishati za kisasa za kupikia.

Kongamano hilo linalenga kupendekeza mikakati ya kufanikisha upatikanaji wa nishati safi, za bei nafuu na endelevu nchini Tanzania.

Kongamano litafanyika tarehe 1 na 2 Novemba 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam na kuwakutanisha watunga sera, wadau wa maendeleo, wajasiriamali, wawekezaji, wafadhili, wanataaluma na wananchi kwa ujumla.

Je, mdau unaweza kutueleza ni vikwazo vipi vinadumaza matumizi ya gesi ya kupikia nchini?
 
Back
Top Bottom