Nelson Kileo
JF-Expert Member
- Oct 29, 2011
- 3,062
- 3,280
Unamuita Drogba wakati Sekta ya mpira ikiwa na matatizo lukuki, ukata mkubwa wa Vifaa na miundombinu ya Michezo Mashuleni na Mitaani, hatuna academy za kutosha nchini.
Suala la Msingi:
Wakati Didier Drogba akilipwa fedha nyingi kama "pambo" la usomaji wa hotuba ya bajeti, sekta ya michezo nchini, Tanzania inateseka kwa ukosefu wa vifaa vya msingi na viwanja bora. Hii inadhihirisha kuwa serikali inatumia fedha nyingi kwenye matokeo yasiyo ya muhimu (sherehe) badala ya kuwekeza kwenye mchakato wa kukuza vipaji (vifaa na walimu)
Ni kejeli kubwa sana na tunaitaka Wizara ya Michezo kuacha kutumia "njia za mkato" za kutafuta sifa kupitia siasa badala yake watafute Mambo yanayoleta matokeo chanya kwa Sekta na kwa Taifa.
Gharama za kumleta na kumlipa Drogba zingeweza kununua maelfu ya mipira ya kisasa, seti za jezi, na vifaa kwa ajili ya shule za msingi na sekondari nchini kote. Kwa sasa, vijana wengi wenye vipaji mitaani wanacheza na mipira ya "karatasi" huku fedha za umma zikitumika kumlipa mchezaji mstaafu wa kigeni kuja kupunga mkono bungeni.
Ni kejeli kuzungumzia maendeleo ya michezo huku tukiwa na shule zisizo na matundu ya vyoo, wanafunzi wasio na mipira ya kufanyia mazoezi, na walimu wa michezo wasio na vifaa. Tunaitaka Wizara ya Michezo kuacha kutumia "njia za mkato" za kutafta sifa kupitia watu maarufu na badala yake iwekeze fedha hizo kwenye mahitaji halisi ya michezo nchini.
Soma Pia: Didier Drogba atinga bungeni kushuhudia uwasilishwaji wa makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Kama ni AFCON Tayari CAF wameshaitangaza vya kutosha.
Hapa kuna uwalakini,
Tuonyeshwe ni kiasi gani kalipwa Drogba kuja Tanzania na ni ipi mikakati chanya ya ujio wake.Pamoja na Utajiri wa Drogba na Umaarufu wake wote tuelezwe ni nini anaacha Tanzania kwenye kusaidia sekta ya michezo baada ya ziara yake hii.
NB: Tuacheni kulitaja Jina la Mungu sana pale tunapofanya Ubaya.