Wakuu naombwa kujuzwa, natakiwa kuwa na vitu gani muhimu ambavyo vitahitajiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri husika au ofisi ya shule. Hii itanisaidia kuviandaa vitu hivyo mapema na kuepusha usumbufu wa kurudi tena nyumbani ili kufuatilia na hatimaye kujikuta napoteza nafasi ya ajira. Nawaomba wazoefu na wajuzi wa hili mnifahamishe.