Ni vitu gani vinahitajika kusajili line ya Safaricom ili niwezi kutumia Paypal?

Ni vitu gani vinahitajika kusajili line ya Safaricom ili niwezi kutumia Paypal?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Habari majirani, Huku kwetu Tz Paypal inaruhusu malipo tu, Haiingizi pesa, Hivyo nimeona mbadala ni kuja hapo mpakani ili nisajiliwe line ya Safaricom ambayo hata huku kwetu inafanya kazi maana wana undugu na Vodacom.

Je, ni vitu gani vinatakiwa ili niweze kupata hio simcard?

Asanteni
 
Pasipoti tu ndio inahitajika jombaa, kwa mgeni, wakenya wana option ya kutumia pasipoti au ID card kusajili SIM card zao. Tena huduma yenyewe kuipata sio lazima ufike hadi mpakani. Hebu ulizia ulizia wenzako kutoka mlimani huko huko Tz watakueleza.

Kuna Dingilai flani hivi wa Arachuga tulikuwa tunawasiliana naye na namba ya Safcom tukiwa kwenye shughuli za kibiashara. Nilipomhoji akaniambia aliisajili Moshi au labda A-Town, sikumbuki vizuri.
 
Ila kaa ukijua ukisajili kwa location ya TZ paypal utapata version ya TZ pia,yan itakuwa haina tofauti na laini yako ya Vodacom
 
Back
Top Bottom