KIXI
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 1,955
- 2,465
Kuna nyumba ya kwanza kupanga nilitamani niwahi kujenga coz ndio nimetoka home nakutana na visa nikaona labda nyumba za kupanga zote zipo hivyo.Nakumbuka miaka hiyo ndio nimepata kazi benki Fulani, nikapata nyumba Sinza ya mama mtu mzima kijana.
Akanikaribisha sana, hakuwa na noma, nilipokuja kununua flat TV enzi hizo plasma tv ndio zimetoka, hamna cha LCD na LED ni ndoto kabisa, yaani ndio kwanza watu wachache sana tumeamza kujikwamua kutoka kwenye machogo.
Basi yule mama akawa anataka muda wote aje ashinde ghetto kwangu, anavaa nguo very light.
Kuna siku jumamosi nimemaliza kufua, nikasema Leo nijilipie, nikachukua Konyagi kubwa, nikawa na Dodoma wine, kwenye oven kilo mbili za kitimoto zinaokwa taratibu. Mara ghafla mlango unagongwa huku mtu akiingia ndani bila kukaribishwa.
Nilikuwa Niko na boksa tu sikuwa natarajia mgeni, akaniudhi sana. Nikakimbilia taulo, akanifuata akanivua taulo. Nikasimama wima hasira Imenijaa.
Akaanza kujiliza ohh Mimi nakupenda siku zote, wewe unajidai huoni.
Nikamkaripia nikamwambia anikome. Baada ya hapo alianza chuki na visa, nilikaa miezi minne tu nikahama.
Kwanza picha linaanza mzee mwenye nyumba kila mwezi anakuja kukagua nyumba anaingia hadi chumbani anakagua kama umetoboa ukuta ni kesi ilikuwa inanikela sana.
Cha pili mimi kazi zangu zilikuwa za kusafili naweza kusafili hata siku mbili sasa kwa usalama nilikuwa naacha taa ya nje inawaka ila nikitoka tu anakuja anafungua taa anaitoa panakua giza nikirudi nakuta taa haipo sasa siku ya kwanza nikajua labda taa wezi wameiba nashaangaa kesho yake nakutana nae ananiuliza umesharudi njoo uchukue taa yako nikamuuliza vipi mzee mbona unatoa taa yangu ananiambia eti taa unaposafiri unaicha wazi inatumalizia umeme wakati pesa ya umeme natoa hata nikiwa nimesafiri umeme ukiisha ananipigia simu kutaka nilipie umeme.
Nilimjibu tu nikiibiwa hapa basi chanzo ni wewe coz taa ndio ulinzi wangu pakiwa giza watu wanajua hakuna mtu hivyo ni rahisi kuibiwa
Swala jingine kama umeacha mlango wazi mzee alikuwa anaingia tu bila hodi ukimuuliza vipi mbona unaingia bila hodi anasema hii ni nyumba yangu.
Unajua gharama niliyotumia kujenga hii nyumba?
ila hakuacha hizo tabia ikabidi nihame tu