Ni wakat sasa hzi njia ziwekewe 4 lane badala ya double lane

Ni wakat sasa hzi njia ziwekewe 4 lane badala ya double lane

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,700
Reaction score
35,783
Sa hv ukiondoka nyumbani kusafri hasa hzi route ndefu , uhakika wa ww kufika salama ni 50/50..

Kwa nchi yetu ajali za Magari mawili kugongana uso Kwa uso ndo habar ya mjini , na route ndefu ndo zinazoongoza Kwa ajali ,
1. DAR - DODOMA -MWANZA
2. DAR - MBEYA
3.DAR - ARUSHA

Kwa sababu ya umaskini wetu bado tunategemea usafr wa gari kuunganisha wakazi wa Dar es salaam na miji hii , kwa umbali uliopo hii ni too dangerous ,kunahtajika miundo mbinu Bora kuweza kufanikisha hili ...miundo mbinu yetu ya barabara bado ni changamoto Sana.

Kwa umbali huu nchi za wenzetu usafr salama ni tren za umeme na aviation , wanajua huwez kuendesha gari Zaid ya km 700 mpak 1200 huko bila kufanya error barabarani , sku zote barabarani error yyte reward yake ni kifo.

Na ndo mana ajari nyingi zaid za barabarani zipo kwenye nchi maskini

Imagine unasafr kutoka Mwanza kuja DSM zaidi ya km 1200 , itakulazimu usafr takrban masaa 15 ukiwa na constant speed 80km/hr , ni mwendo wa hatari kama njia ni nyembamba inayokulazimu ufanye overtaking mara Kwa mara , wakat mwingine unakutana na msururu wa malori ma 4 au ma 5 , yanayoenda constant speed ya Kobe , ukicopy unachelewa inabd ufanye namna uyapite yote with high speed, Njia nzima itakulazimu ufanye hivi zaid ya mara kumi, kiukweli ni hatar Sana, chance ya kugongana uso Kwa uso ni kugusa tuu

Inavyoonekana kwenye nchi yetu hakuna tumaini lolote la mtandao wa treni ya umeme kuanza kufanya kaz kwenye hii miji mikubwa , aviation industry na yenyewe inachechemea na Gharama ni kubwa ...

Nashauri hzi njia ndefu ziongezewe upana wa barabara uwe 4 lanes badala ya 2 lanes , hata kama traffick watabaki kufanya regulation ya speed barabarani , ittapunguza pia uwezekano wa kugongana uso Kwa uso ....

Maendeleo bila usalama wa raia ni hamna kitu.

unnamed+(9).jpg


dhk-ctg.jpg
 
Naunga mkono hpja ila UMASKINI ndo gonjwa letu just imagine hata hii route ya DAR-MZA imekuja kukamilika full lami mwaka 2014 hapo ndo ilikua lami 100% tokea uhuru sasa imagine wakuzikamilisha izo 4 way kwa sasa atakamilisha lini??
 
Hoja nzuri sana hii, lakini kwa huu uchumi wetu wa kuungaunga hata waanze tuu na barabara zenye 3 lanes... yaani hizi 2 lanes za sasa waongeze another lane ili ziwe tatu. Yaani hii ndiyo solution kwa hizi ajali za kila siku.
 
Hoja yako nimeiongelea mara nyingi humu ila sidhani kama tuko kwenye nafasi ya kufanya upanuzi sasa hivi wala miaka ya hivi karibuni ila uhitaji upo sana.

Shida tunachakachua mipango ya miradi hii. Sidhani kama utaleta mkandarasi wa nje akuchoree ramani ya long distance road kama hizo halafu aweke lanes mbili, hawezi kushauri hivyo. Hii ni sisi wenyewe tunachakachua mipangilio inakuja kutucost baadae. Utasikia wanakwambia afadhali tujenge barabara nyingi kwanza tutakuja kupanua baadae. Ndiyo maana tunajenga barabara hazina mitaro wakati mitaro kawaida huwa ni sehemu ya mikataba ya ujenzi wa barabara.

Kiukweli hizo trip ulidhohorodhesha siyo mbali kama tunavyodhani na usafiri wa magari unafaa kabisa. Kwa lanes 4, kukiwa na kitenganishi katikati speed limit ingekuwa hata kilometer 120 kwa saa na bado ingekuwa salama. Mwanza ni umbali wa masaa 5 tu.
 
Back
Top Bottom